Na.Khadija Seif, Michuziblog
BENDI ya Msondo Ngoma yawaalika Mashabiki zake kuhudhuria Tamasha la Miaka 60 tangu kuanzishwa kwa bendi hiyo.
Akizungumza na Wanahabari Leo Oktoba 04,2024 Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Kamati ya Tamasha hilo Said Kibiriti amesema bendi hiyo imekuwa Mfano wa kuigwa katika tasnia ya Muziki kutokana na kuhudumu kwa Miaka mingi na kuzaliwa kwa vipaji vingi vizuri.
Aidha Kibiriti amesema Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika Oktoba 26,2024 katika ukumbi wa Gwambina uliopo Jijini Dar es Salaam.
"Tamasha litafanyika Ukumbi wa Gwambina ambapo Wanamuziki mbalimbali watasindikiza sherehe hizi ambapo pia bendi kama Bogoss ikiongozwa na Rais wa Milele Nyoshi El sadat ,Charles Baba,Fresh Jumbe na Wengine wengi watatumbuiza."
Kibiriti ameongeza kuwa Bendi hiyo itafanya Kisomo kwa ajili ya Kurehemu Wanamuziki waliowahi kuhudumu katika bendi hiyo ambao kwa sasa Wametangulia mbele ya Haki.
Kwa upande wake Rais wa bendi ya Bogoss Nyoshi El sadat amesema anaona fahari kupanda Jukwaa moja na Wanamuziki tofauti tofauti akimtaja zaidi Fresh Jumbe .
"Nimeifahamu bendi hii Miaka ya 90 na Natamani siku ya Tamasha niweze kuimba wimbo "Tuma" ili kusherehesha zaidi miaka hiyo 60 ya bendi Kongwe".
Naye Juma Katundu maarufu kama 'JK' amesema kuwa ni kitu kikubwa kwa watanzania kujitokeza kwa wingi na kutoa ushirikiano siku hiyo kwani Waimbaji wanaendelea na Mazoezi.
Tamasha la Miaka 60 ya Msondo litasindikizwa na Twanga Pepeta, Ally Choki, Nyoshi El Sadati Rais wa Milele, Spidoch Band 'Wazungu weusi' pamoja na msanii wa Bongo fleva Bernard Paul 'Ben Paul huku wakipewa sapoti kutoka bendi ya Dar modern taarab.
Tamasha la miaka 60 kiingilio ni Laki moja, Elfu 50 na kawaida 15000 ukichukua tiketi yako mapema kwa mlangoni kiingilio ni Elfu 20
Mwenyekiti wa Tamasha La Kuadhimisha Miaka 60 ya Bendi ya Msondo Ngoma Said Kibiriti akizungumza na Wanahabari Leo Oktoba 04,2024 Jijini Dar es Salaam mara baada ya kutangaza rasmi tamasha hilo ambapo litafanyika Oktoba 26,2024 Ukumbi wa Gwambina Jijini Dar es Salaam na Kushereheshwa na Wanamuziki mbalimbali akiwemo Fresh Jumbe kutoka Sikinde OG, Charles Baba kutoka Twangapepeta pamoja na Allychoki
Mwananamuziki kutoka Bendi ya Twangapepeta Charles Baba akizungumza machache mara baada ya kutangazwa ujio wa Tamasha La Kuadhimisha Miaka 60 ya Bendi ya Msondo Ngoma akihaidi Mashabiki kukonga nyoyo zao kwa kutumbuiza vibao vilivotungwa na bendi hiyo ya Msondo Ngoma
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...