Na Mwandishi wetu- Dodoma

Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu na Taasisi ya Mpango wa Biashara wa Kimataifa (IBI) zimesaini makubaliano kuhusu mashirikiano katika masuala ya Ufuatiliaji na Tathmini.

Makubaliano hayo yamesainiwa leo tarehe 08 Oktoba 2024 katika ukumbi wa ofisi hiyo ambapo mara baada ya kutia saini, Katibu Mkuu katika ofisi hiyo Dkt. Jim Yonazi amebainisha kuwa, lengo la kuanzisha mfumo wa tathmini na ufuatiliaji ikiwa ni kuhakikisha nchi inasonga mbele katika suala la tathimini na ufuatiliaji wa miradi yote ya serikali.

Dkt. Yonazi ameongeza kuwa ili kuweka mipango inayotekelezeka na kutoa matokeo chanya ipo haja ya vitengo vilivyoanzishwa kujengewa uwezo, jukumu ambalo huratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, huku akiwahimiza wadau wengine kuiunga mkono Serikali hatua iliyofanywa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) kwa kutoa ufadhili katika taasisi hiyo katika kuisaidia Serikali kwa kazi ya tathimini na ufuatiliaji.

“Tumeingia makubaliano na wadau kwa ajili ya kushirikiana katika kujenga uwezo wa ufuatiliaji na tathmini serikalini, ikiwa ni uamuzi wa serikali kuanzisha mfumo wa ufuatiliaji na vitengo katika serikali, hivyo ni lazima kujengewa uwezo jukumu ambalo limekabidhiwa katika Ofisi ya Waziri Mkuu la kufuatilia na kutathimini utendaji wa serikali nchi nzima,” alisema Dkt. Yonazi.

Aidha Dkt. Yonazi aliwahimiza wadau wengine wa maendeleo kujitokeza kuiunga mkono Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia kada ya ufuatiliaji na tathmini kuhakikisha shughuli za serikali zinafanyika na kuleta matokeo yanayokusudiwa.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...