NA WILLIUM PAUL, MOSHI.

MKUU wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amesema kuwa maandalizi ya kuelekea kwenye zoezi la uandikishaji wananchi katika Daftari la mkazi litakaloanza kesho yamekamilika ambapo jumla ya vituo 2368 vitatumika.

Babu ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake ambapo alisema kuwa, mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi wa Serikali za mitaa ambapo wananchi wanaenda kuchagua viongozi wa Vijiji, vitongoji, mitaa pamoja na wajumbe wa Serikali za Vijiji na mitaa.

Alisema kuwa, uchaguzi huo utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu ni takwa la Kikatiba na kisheria ambapo inawataka kuchagua viongozi wa Serikali za mitaa kila baada ya miaka mitano.

"Nchi yetu ni nchi ya uhuru na kidemokrasia ambapo wananchi wanapaswa kuamua kuhusiana na namna ya kuendesha masuala ya msingi kuhusiana na Serikali zao kwa muktadha huo na kwa kuzingatia na kuheshimu misingi ya demokrasia wananchi wanahaki ya kushiriki katika uchaguzi na kumchagua kiongozi wanayemtaka" Alisema Babu.

Alisema kuwa, zoezi la kujiandikisha litaanza Oktoba 11 hadi 20 mwaka huu ambapo vituo vitafunguliwa kuanzia saa mbili asubuhi na kufungwa saa kumi na mbili za jioni.

Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa, sifa za wananchi watakaojiandikisha katika Daftari hilo la mkazi ni awe Rai wa Tanzania, umri wa kuanzia miaka 18 na zaidi pia awe mkazi wa kijiji au kitongoji au mtaa ambao uchaguzi unafanyika, awe na akili timamu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...