Na Mwandishi wetu Mpapura,
Afisa Tarafa Mpapura Emmanuel Shilatu amesisitiza jamii kuhakikisha makundi maalum yanapewa nafasi ya kuchagua na kuchaguliwa kwenye uchaguzi huu wa Serikali za mitaa 2024.
Gavana Shilatu aliyasema hayo kwenye mikutano na vikao alivyofanya ya kuhimiza ushiriki kikamilifu wa Watu kwenye mazoezi ya kujiandikisha na kupiga kura.
"Kumekuwa na tabia kwenye jamii kuwaweka nyuma ama pembeni Watu wa makundi maalum wasishiriki uchaguzi, jambo ambalo sio sahihi. Kama Wana akili timamu na sifa zote takiwa wanazo, uzee ama ulemavu wao sio kigezo cha kutojiandikisha ama kutochagua ama kuchaguliwa. Jamii ihakikishe inawashirikisha na kuwapa nafasi kikamilifu kwenye uchaguzi huu wa Serikali za mitaa." Alisema Gavana Shilatu
Kwa upande wake Gavana Shilatu alihaidi kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi kwa kujiandikisha zoezi litakaloanza tarehe 11 - 20/10/2024 na kupiga kura kwenye uchaguzi unaotarajia kufanyika 27 Novemba, 2024

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...