~ Aeleza Kuna maisha baada ya uchaguzi
Na Mwandishi wetu Mpapura
Afisa Tarafa Mpapura Emmanuel Shilatu amewataka Wananchi kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa na Vijiji kikamilifu na kwa amani na utulivu.
Tahadhari hiyo imetolewa na Gavana Shilatu kwenye mkutano na Wananchi uliofanyika Kijiji cha Mnyundo kilichopo Kata ya Ndumbwe.
"Tarafa nzima hakuna viashiria vya uvunjifu wa amani, ni vyema tuendelee kudumisha amani na Usalama kwenye maeneo yetu nyakati zote za uchaguzi. Tufanye siasa za kistaarabu, tujiandikishe kwa amani na tupige kura kwa utulivu. Muhimu tutambue kuna maisha baada ya uchaguzi, tahadhari na umakini ni muhimu ." Alisema Gavana Shilatu
Nae Mzee Hamis ambaye ni Mwananchi wa siku nyingi wa Mnyundo amewaambia Tanzania ya sasa si kama ya zamani, Kuna maendeleo makubwa na hayo yote ni matokeo ya uwepo wa amani nchini.
"Nina miaka mingi, nimeona awamu zote Tanzania ya sasa imepiga hatua kubwa. Hii yote ni kwa sababu ya misingi mizuri ya amani na utulivu tuliyo nayo, tulinde amani yetu ni tunu kubwa ya maendeleo." Alisema Mzee Hamisa akiwaasa Wananchi waliohudhulia Mkutano huo.
Gavana Shilatu yupo kwenye ziara ya kitarafa ya kufanya vikao na mikutano ya kuhamasisha Wananchi kushiriki uchaguzi kwa amani na utulivu

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...