Mwenyekiti wa mtaa wa Namanyigu kata ya Mshangano manispaa ya Songea Abdulkadri Myao, amesema Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Songea SOUWASA, wameboresha kwa kiasi kikubwa huduma wanazozitoa ukilinganisha na kipindi cha nyuma jambo ambalo limerejesha matumaini kwa wakazi wa eneo hilo.
Amebaisha hayo baada ya SOUWASA kutembelea mtaa huo ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya Mtaa kwa Mtaa inayotekelezwa na Mamlaka hiyo katika kipindi cha wiki ya huduma kwa wateja, ameonyesha kufurahishwa na huduma inayotolewa kwasasa ambayo amesema asilimia kubwa ya wakazi wa Namanyigu waliyofikiwa na miundombinu ya maji wanatumia huduma hiyo.
Myao amepongeza jitihada za SOUWASA kutoa huduma ya maji katika mtaa wake, huku rai yake kubwa nikusaidia kusogeza huduma hiyo katika maeneo yaliyosalia ili kuhakikisha kwa ujumla wao wanapata maji safi na salama nakuepuka kutumia maji ya visima.
Wakizungumza wakazi wa Mshangano Ibrahim Adam pamoja na Fadhila Mohamed wameelezea utofauti mkubwa uliokuwepo kipindi cha nyuma na jinsi hali ya huduma ilivyo hivi Sasa, ambayo wamesema imeboreshwa kwa kiwango kikubwa nakushauri hata kipindi cha kiangazi hali ya upatikanaji wa maji iendelee kutolewa vizuri ili kupunguza changamoto ya kutafuta njia mbadala kupata maji.
Akizungumza na waandishi habari baada ya kusikiliza kero za wananchi Mhandisi uzalishaji na usambazaji kutoka SOUWASA Charles Kitavile, amesema kwa sasa mamlaka imeandaa mkakati maalumu wa kuhakikisha wananchi wote wa kata ya mshangano ambao hawajapata huduma ya maji safi wanafikiwa na huduma ya maji
Kutokana na wananchi wengi kuwa na hofu ya kuunganishiwa huduma ya maji kwa kuhofia gharama, katika kampeni ya SOUWASA mtaa kwa mtaa, Mkuu wa Kanda kitengo cha Biashara kutoka SOUWASA Juma Mwakaje ametoa elimu kwa wananchi amesema gharama za kuunganishiwa huduma za maji zinatofautiana kwa kila mteja hii nikutokana na umbali kutoka katika miundombinu ya bomba kubwa la maji lilipopita, hivyo gharama zitajulikana baada ya wataalamu kufika na kupima umbali huo.
Kampeni ya SOUWASA mtaa kwa mtaa imepokelewa vizuri katika maeneo yote waliyotembelea ambapo kongole zimetolewa kwa Mamlaka hiyo hususani kuondoa changamoto ya kukatikakatika kwa maji jambo ambalo limechochea hamasa kubwa kuongeza wateja wapya.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...