NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

TIMU ya Taifa ya Tanzania imeshindwa kutamba katika dimba lake la nyumbani mara baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya timu ya Taifa ya Congo DR.

Katika mchezo huo wa kufuzu AFCON 2025 ulipigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam, timu zote zilicheza soka safi, licha ya Congo DR kutengeneza nafasi nyingi za mabao bila mafanikio kwenye kipindi cha kwanza.

Mpaka mapumziko mechi ilikuwa 0-0, hadi kipindi cha pili timu zote ziliweza kufanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji ili kuweza kupata matokeo, lakini bahati ilikuwa kwa Congo DR ambao walimtoa Silas na nafsi yake kuchukuliwa na Meschack Elia ambaye aliweza kupachika mabao mawili ambayo yaliiwezesha Congo DR kuondoka na ushindi kwenye mchezo huo.

Congo DR iliweza kupata mabao kupitia kwa Elia dakika ya 88 ya mchezo pamoja na dakika nne za nyongeza na matokeo kuwa 2-0.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...