Na mwandishi wetu, Dubai

MRADI wa Tanzania Digital Inclusion Project unatekelezwa na shirika la Internet Society Tanzania(ISOC-TZ) katika umetwaa tuzo ya uwezo mifumo ya majiji janjaduniani (Smart city).

Mradi huo kwa Tanzania unatekelezwa Jijini Dar es salaam, Mwanza na Kiliamnjaro.

Tuzo hizo zilizofanyika Dubai, Rais wa Shirika la ISOC-TZ, Nazar Kirama alipokea tuzo hiyo alisema huu ni uthibitisho kwa kuna mambo mazuri yanayofanyika nchini Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Alisema sera nzuri zinazotekelezwa na serikali ya Tanzania ndio zinazofanya watanzania katika sekta ya Civil Societies kupaisha kazi zetu.

"Mfumo wasera ya serikali iliyowezesha kuweka mkonga wa taifa wa kilomita zaidi ya 12000 nchi nzima imetuwezesha kuunganisha shule 15 na serikali huduma ya kimtandao ya kasi." alisema Nicholas

Aliongeza msingi wa sera pia unatokana na ilani ya chama tawala ambapo ni Chama cha Mapinduzi (CCM ) kupitia ukurasa wake wa 98 wa ilani yake ya mwaka 2020 - 2025.

Alisema malengo ya mradi ifikapo mwaka 2034 ni kuwa na Community Network Hubs 200 Tanzania nzima ili kuunganisha watu million 4 na mtandao wa kasi na kutoa Elimu digiti kwa vijana na wanawake Wajasiriamali milioni 1.5.
 

Rais wa ISOC-Tanzania Nazar Kirama wa kwanza kutoka kushoto akiwa na wadau wa mawasiliano katika mkutano wa Tuzo baada ya kujenga mifumo Janja ya katika Majiji nchini Tanzania.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...