]


Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kupitia Idara ya Kazi, imetoa elimu ya sheria za kazi kwa Wafanyakazi na Waajiri wa sekta za ulinzi Jijini Dar es salaam.

Akizungumza Kamishna wa Kazi, Suzan Mkangwa amesema kuwa dhumuni la semina hiyo ni kutoa Elimu ya Sheria za Kazi katika Sekta ya Ulinzi nchini ili kuendelea kupunguza changamoto zinazowakabili baadhi ya wafanyakazi katika Sekta hiyo

Aidha, Mkangwa amebainisha baadhi ya malalamiko ambayo yamekuwa yakiripotiwa Idara ya kazi ikiwemo wafanyakazi kuajiriwa bila mikataba, Waajiri kutowasilisha michango katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na kuachishwa kazi kiholela bila kuzingatia sheria za kazi.

"Ni matumaini yangu semina hii itakwenda kuondoa changamoto za ukiukwaji wa sheria za kazi ambazo zimekuwa zikiripotiwa ofisini mara kwa mara" amesema.

Awali akizungumza Afisa Matekelezo kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Asha Udindo ametoa rai kwa Waajiri wa sekta hizo  kujiunga WCF na kuwasilisha michango kwa wakati ili kulinda haki zao dhidi ya majanga yanayoweza kuwapata wafanyakazi wao wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kila siku.

Naye, Meneja Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Dar es salaam Feruzi Mtika amesema Serikali haitawavumilia waajiri wote wa sekta binafsi ambao wanakata michango ya wafanyakazi wao bila kuiwasilisha katika Mfuko huo.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...