WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzani (TFS) umewataka watanzania kuchangamkia fursa ya Utalii wa Nyuki, kutumia sumu ya nyuki kama tiba mbadala ya magonjwa mbalimbali ya kuambukizwa na yasiyoambukizwa.
Mhifadhi Mwandamizi wa TFS kutoka Shamba la Miti Silayo, Juma Mdoe  amefafanua hayo wakati akitoa elimu mbele ya wananchi katika Maonesho ya Saba ya Teknolojia ya Madini mjini Geita.

Alisema tafiti zinaonesha kuwa sumu ya nyuki ina mchanganyiko wa kampaundi nyingi zilizotengenezwa na nyuki ambapo mwilini mwa binadamu inasaidia kumkinga na vimelea vya magonjwa mbalimbali. 

Lisa Richard mkazi wa Mkoa wa Geita ambaye anafanya kazi Benki ya CRDB amesema hii ni mara ya 3 kufika Banda la Maliasili na kutumia Tiba hiyo ya kudungwa na Nyuki na amesema kwake inamsaidia kujikinga na maradhi na baada ya kutumia njia hiyo ya Tiba ya Nyuki atakuwa anafanya mara kwa mara peke yake kwa kuzingatia maelekezo ya wataalam wa ufugaji nyuki kwa kuwa elimu hiyo imemsaidia baada ya kufika katika Banda la Maliasili.
Teris Gogo Mkazi wa Mji wa Geita amesema yeye licha ya kufika katika Banda hilo alikuwa na utaratibu huo ila elimu aliyopata kutoka kwa maafisa wa Banda la Maliasili imempa chachu ya kuendelea kutumia Tiba hiyo ya nyuki kutokana na elimu aliyopata kwenye Banda hilo.








 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...