Wakuu wa Polisi wa nchi za Afrika Mashariki na kati kutoka nchi sita wameahidi kushirikiana kupamba na matukio ya uhalifu mtandaoni kwani yameonekana kushika kasi.

Akizungumza leo Oktoba 25 2024 jijini Dar es Salaam katika mkutano wa nane wa wakuu wa polisi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa niaba vya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, Camilius Wambura, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini (DCI) Ramadhani Kingai alisema mbali na matukio mtandaoni kushika kasi na kuvuka mipaka Tanzania haina matukio makubwa ya mtandao.

Alisema lengo kuu la mkutano huo ni kujadili mambo mbalimbali ya kiusalama hasa uhalifu unaovuka mipaka sasa ili kuyadhibiti matukio hayo nchi hizo zinatakiwa kuendeleza ushirikiano uliopo kwa kushirikishana taarifa.

“Tanzania hatuna matukiuo makubwa ya mtandao zaidi ya watu kubahatisha na hiyo inatokana na kufanyika kwa operesheni kubwa na nyingi mara kwa mara ambazo zimesababisha wahalifu kukamatwa na kufikishwa mahakamani.

“Zamani kulikuwa na shida kidogo mtu ukishare taarifa inayohusiana na uhalifu mtu anaona unatoa siri, lakini katika uhalifu unavuka mipaka huwezi ukajifungia na kupata suluhu ya uhalifu uliotokea wewe mwenyewe mpaka uende kwa mwenzako na upite mpaka," Kamishna Kingai.

Uhalifu kwa mfano wa makosa ya kimtandao mtu anakuwa yupo nyumbani na anaiba benki kupitia simu ya mkononi kwa mtu yupo Uganda anaiba Tanzania, sasa uhalifu huu watautaumudu kwa kushirikishana taarifa na kuwafanya watu wetu kuwa na uelewa,” alisema.

Alisema uhalifu huo ni mpya na zamani haukuwepo hivyo Watanzania walikuwa wanaufahamu uhalifu wa zamani hivyo wanatakiwa kujifunza mbinu mpya za kupambana na uhalifu huo.

“ Kwa mfano kwa nchi za Afrika Mashariki uhalifu unaoleta shida ni uhalifu wa mitandaoni na viashiria vya ugaidi kwa juhudi kubwa zinazoendelea za wakuu wa nchi na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana baina ya nchi za Afrika Mashariki wahusika hawa hawapati muda wa kujipanga na kufanya uhalifu huu,” alisema.

Alisema kwa jinsi wanavyojipanga kudhibiti kunawawezesha kuwa katika nafasi nzuri ya kuwahudumia wananchi kwa usalama.

Kamishina Kingai akizungumzia mkutano huo alisema lengo ni kujadili mambo mbalimbali ya kiusalama hasa uhalifu unaovuka mipaka.

“Kwa mfano uhalifu wa human traffic, ugaidi na uhalifu mwingine ambao unavuka mipaka, tutajadili mambo mengine yaliyojadiliwa mwaka jana jinsi yalivyoshughulikiwa, kuangalia sera mbalimbali zinazohusiana na kazi za polisi na taasisi nyingine,”alisema.

Kingai alisema jumla ya nchi sita zimekutana kuhakikisha ardhi ya Afrika Mashariki inakuwa salama.

“Hali ya udhibiti matukio ya uhalifu wa kuvuka mipaka ni nzuri kwa sababu tunashirikiana na kushare taarifa kati ya nchi na nchi, kati ya idara moja ya serikali na nyingine lakini kushare experience mambo ambayo wenzetu wamefanikiwa na kuhakikisha wahalifu hawajitanui na kuwashughulikia kadri inavyopaswa wananchi wa Afrika Mashariki wazidi kuwa salama,”alisema.

Kutokana na jitihada hizo, Kingai aliishukuru Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuichagua Tanzania kufanya mkutano huo kwani inatokana na nchi kuwa salama.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Thomas Jal Thomas kutoka nchi ya Sudan ya Kusini, alisema wamekutana kuangalia jinsi ya kupambana na makosa ya kimtandao yanayovuka mipaka .

“Kupitia kikao hiki tutaangalia nini kifanyike kudhibiti matukio hayo kuwasaidia waathirika wa matukio hayo jinsi ya kuyashughulikia, ninawashukuru washiriki wa mkutano huo kwani watakachojadili kitaleta manufaa kwa mstakabadhi wa nchi zetu,” alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...