Katika kuadhimisha siku ya afya ya macho duniani Jumla ya Wananchi 10,378 Mkoani Lindi wamefikiwa na huduma ya Afya ya macho ambapo kati yao 9690 wamefanyiwa vipimo na kupatiwa matibabu katika maeneo tofauti ya Mkoa huo.
Akizungumza katika maadhimisho hayo ya Afya ya macho Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi Sokoine Dkt. Sharifu Hamza amesema zoezi hilo limeendeshwa kwa ufadhiri wa mashirika ya Heart to Heart foundation,CBM pamoja na Korea church .
Amesema zoezi hilo limendeshwa kwa siku saba kuanzia oktoba 4 hadi 7 na wataalamu walipita katika shule mbalimbali kwa halmashauri zote sita kutoa elimu pamoja na kutoa matibabu kwa wananchi walioonekana na changamoto ya afya ya macho.
Afisa mradi kutoka shirika la heart to haert foundation Edward Aloyce amesema shirika lao limekuwa likifanya mradi wa macho katika Mkoa wa Lindi wakilenga kupata watoto 20 wenye changamoto ya mtoto wa jicho ambao watanufaika kufanyiwa oparesheni bure.
Hata hivyo Aloyce ametoa wito kwa Wazazi na walezi Mkoani humo kujenga tabia ya kuwahimiza watoto kufanya uchunguzi wa changamoto ya macho ili kulinda afya za macho lakini kufanya wadau hao kuweza kuwasiliana na wataalam wa hospitali ya muhimbili kuja kuwasaidia kimatibabu yakibingwa zaidi.
Amesema ni faraja kwao kuona zoezi hilo kwa Mkoa wa Lindi linefanikiwa kufanyika kwa kiasi kikubwa na mafanikio makubwa
Dkt. Mwita Machaja ni mtaalamu wa magonjwa ya macho Hospital ya Rufaa ya Lindi Sokoine amesema zipo sababu mbalimbali zinazopelekea matatizo ya macho ambapo miongoni kwa sababu hizo ni umri, ajali, lishe duni , maambukizi na sababu za kuzaliwa.
Amesema sababu kubwa inayowafanya baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Lindi kupata changamoto ya macho ni kukosa lishe bora hali inayopelekea kuathirika kwa macho.
"wakazi wengi wa Lindi wanaopata changamoto ya macho inatokana na kutokula vyakula vinavyolinda macho uwenda kwa kujua ama kutokujua kula mboga za majani zilizoiva sana ama pengine kutokula kabisa"Alisema Dkt Mwita.
Nae Asha Matola mkazi wa Lindi amesema amefika hospitalini hapo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi zaidi baada ya kuugua macho kwa muda mrefu na kwamba imani yake atapata matibabu mazuri.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...