Na Mwandishi Wetu


WATUMISHI Housing Investments (WHI) imetunukiwa tuzo ya Nyumba za gharama nafuu zaidi Afrika iliyotolewa na Taasisi ya Mikopo ya Nyumba Afrika (Africa Union for Housing Finance-AUHF) inayo tambuliwa na Umoja wa Afrika (Africa Union).
Tuzo hiyo imetolewa katika Mutano Muu wa AUHF mwaka 2024 uliofanyika Zanzibar hivi karibuni na kwamba tuzo hiyo ya heshima inatambua jukumu la WHI katika kuwezesha umiliki wa nyumba kwa watu wa kipato cha chini na kati nchini Tanzania.

Pia kutambua  juhudi zilizofanywa na WHI katika kuleta suluhisho la njia nafuu za malipo za nyumba ikiwemo malipo endelevu yanayolipwa kipindi cha ujenzi bila riba pamoja na utaratibu wa mpangaji munuzi ambavyo vilitaja kama sababu kuu za ushindi huu. 

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na na Kitengo cha Mawasiliano WHI imesema nyumba za WHI zinauzwa kwa bei nafuu kwa kati ya asilimia 10 hadi asilimia 30 ikilinganishwa na nyumba kama hizo kwenye soko, huku bei ya kununua nyumba ikianzia Sh.milioni 38.

Imesema kuwa bei hizo pamoja na njia nafuu za malipo zimewasaidia Watanzania wengi kufikia ndoto zao za kumiliki nyumba. Tuzo hiyo pia inasherehekea kipindi maalum kwa WHI, kwani inatimiza miaka 10 ya ubunifu na ongozi katika sekta ya Makazi.

"WHI inakuwa taasisi ya kwanza nchini na Afrika Mashariki kupokea Tuzo hii ya heshima. WHI imeibuka kinara kutoka kwa taasisi mbalimbali zinazohusiana na sekta ya makazi kutoka mataifa
mbalimbali barani Afrika.

"Tuzo za AUHF zinatambua michango thabiti ya kuendeleza sekta ya makazi barani Afrika. Ushindi wa WHI ulitokana na utekelezaji wake wa kipekee katika kubuni na kutekeleza miradi ya nyumba yenye gharama nafuu zaidi na hivyo kuleta unafuu kwa wanunuzi ikiwalenga watumishi wa umma na wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii."imesema taarifa hiyo.

Aidha, imesema tathmini ilihusisha kuangalia kazi halisi iliyotekelezwa na WHI, pamoja na mazungumzo ya moja kwa moja na wanufaika wa miradi yake. Hiyo  ilitoa fursa ya kupata maoni ya moja kwa moja kutoka kwa wananchi waliofaidika na miradi ya makazi ya WHI, ambapo walielezea jinsi njia nafuu za malipo zimewasaidia kufikia ndoto yao ya kumiliki nyumba.

Imeelezwa AUHF, shirika muhimu linalounganisha wadau wa makazi barani Afrika kwa zaidi ya miaka 40, linawezesha washirika wake kuendeleza fumbuzi zaidi wa makazi ya bei nafuu.

Hata hivyo ahadi ya WHI ya kupunguza gharama za makazi na kutoa njia mbadala za malipo ilionekana kama hatua kubwa kuelekea kufikia maono hayo na tuzo hiyo ni uthibitisho wa dhamira ya Serikali kupitia Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora katika kuwawezesha wananchi wake kupata makazi nafuu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investment (WHI)  Dkt. Fred Msemwa (kushoto) akizungumza na Waandishi wa habari  leo  jijini Dar es Salaam kuhusu Tuzo walioshinda ya Nyumba za gharama nafuu zaidi Afrika iliyotolewa na Taasisi ya Mikopo ya Nyumba Afrika (Africa Union for Housing Finance – AUHF) inayo tambuliwa na Umoja wa Afrika. (kulia )Mkuu wa Idara ya Masoko na Mauzo wa WHI,Raphael Mwabuponde.
(PICHA ZOTE NA  NA EMMANUEL MASSAKA, MICHUZI TV)


Mkuu wa Idara ya Masoko na Mauzo wa WHI Raphael Mwabuponde akitoa shukrani kwa wadau mbalimbali kwa kutoa ushirikiano katika uekelezaji wa majukumu ya WHI tangu kuanzishwa kwake.

Afisa Uhusiano na Masoko Mwandamizi wa WHI Maryjane Makawia (kulia) akitoa ufafanuzi wa jambo kuhusu  WHI ilivyoshinda Tuzo ya Nyumba za gharama nafuu zaidi Afrika iliyotolewa na Taasisi ya Mikopo ya Nyumba Afrika (Africa Union for Housing Finance – AUHF) inayo tambuliwa na Umoja wa Afrika. (kushoto)Mkurugenzi Mtendaji wa WHI Dkt. Fred Msemwa.  PICHA NA EMMANUEL MASSAKA, MICHUZI TV)

Mkutano ukiendelea PICHA NA EMMANUEL MASSAKA, MICHUZI TV)


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...