NA FARIDA MANGUBE 

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe amesema ipo haja ya kuwa na mijadala mahususi ya kitaifa kujadili masuala mtambuka juu ya muundo wa sekta ya kilimo ili kuona namna bora ya kuwezesha kundi la vijana kujihusisha kikamilifu katika shughuli za kilimo.

Aidha Mhe. Bashe amesema taifa linakitegemea Chuo Kikuu  cha Sokoine cha Kilimo kuendesha mijadala ya aina hiyo kwani ndilo chimbuko la wataalamu wa kilimo na vijana zaidi ya mia mbili wa BBT wanaopelekea kufanya mabadiliko makubwa kwenye sekta ya kilimo kupitia mpango huo.

“Kwa sasa tunawatazama vijana hawa kwa jicho la kipekee kutokana na matokeo ambayo tayari tumekishwa kuanza kuyaona kwao na tuna mpango wa kuwafanya vijana hawa kuwa wao ndio watakao kuwa wanagawa mbegu na pembejeo nyingine kwa wakulima kutokana na kuonesha uaminifu mkubwa kwa serikali “amesema Mhe.  Bashe.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Prof. Raphael Chibunda ametumia fursa ya hafla hiyo kuiomba serikali ibadilishe sheria na kanuni za mazingira  zinazohusu Bioteknolojia mbegu za GMO ili isiwabane watafiti na kuruhusu watafiti hao kufanya utafiti kwa uhuru ili kuleta matokeo chanya kwenye sekta ya kilimo.

“Kanuni zilizopo kwa sasa kupitia sheria ya mazingira zinasema kwamba endapo litatokea tatizo lolote litakalosababishwa na mbegu ya aina hiyo mtafiti atawajibika moja kwa moja juu ya tatizo hilo hali ambayo inawakatisha tamaa watafiti” Prof. Chibunda amesema.

Mhandisi Tito Edimund ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vijana Kilimo  Biashara wilaya ya Mvomero amemuomba Mhe. Waziri Bashe kuwa serikali iwawezesha vijana ambao hawamo katika mfumo wa BBT kifedha ili wafanye kilimo chenye tija kuliko ilivyo sasa.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...