ELIMU ya Usalama barabarani haina budi kuwa ya lazima kutolewa kwa wanafunzi na ianzie ngazi ya chini yaani shule ya msingi ili kusaidia watoto kuondokana na changamoto ya ajali zinaweza kuwatokea wanapotoka majumbani kuelekea shuleni au shuleni kurudi nyumbani.

Ameyasema hayo Novemba 5, 2024 Jijini Dar es salaam Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Wakili mwanasheria wa kikosi cha Usalama Barabarani Deus Sokoni wakati akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Alhasan Mwinyi iliyopo Kinondoni kutekeleza Mradia wa Assessment project kwa kushirikiana na chama cha mbio za magari ( Automobile Association AAT)ukiwa na lengo la kutoa elimu ya kuwajengea watoto wa shule za msingi na Sekondari namna ya kuishi kwa usalama wakiwa salama barabarani bila kupata dhara lolote.

" Mradi huu tumekuwa tukiufanya kwa kushirikiana na wadau wa Chama cha mbio za magari (Automobile Association Tanzania AAT ) kwenda nao katika shule mbalimbali na tulianzia Wilaya ya Temeke sambamba na Kikosi cha Usalama barabarani kwani kufanya hivi tunareje maelekezo ya Serikali kuwa elimu ya Usalama barabarani ianzie ngazi ya chini kabisa" amesema Marakibu Deus

Hata hivyo amesema wamewapatia elimu itakayowasidia kukua na kufahamu ni kosa kisheria kukubali kupanda bodaboda moja watu zaidi ya wanne kwani kumekuwa na tabia ya baadhi ya wazazi wamekuwa wakichangishana fedha ili watoto waende shule alfajiri na wamekuwa wakikamatwa na polisi bodaboda wakijetetea uchumi wa wazazi wao hauruhusu kupanda pikipiki moja wanafunzi wawili .

Sambamba na hayo Mrakibu amebainisha kuwa licha ya kuwapatia elimu ya Usalamaa barabarani pia wamewapatia elimu ya usalama barabarani namna ya kuepukana na vitendo vya ukatili wa kijinsia wanavyoweza kutendewa na waendesha magari au pikipiki kwani kuna watu ambao siyo waaminifu wamekuwa na tamaa wakiwarubuni na kuwatendea vitendo ikiwemo ulawiti, ubakaji, hivyo kuwapelekea wengine kukatiza ndoto zao za kimasomo .

Kwa upande wake Athumani Kasanga Meneja wa kukuza biashara AAT chama cha mashindano ya magari amesema wamekuwa wakienda katika mashule mbalimbali kuangalia hali ya miundombinu na kujenga barabara zenye alama(Zebra cross) kwa kushirikiana na kikosi cha usalama huku wakitoa mafunzo namna ya kutumia barabara wasipate madhara yeyote wanapoenda shule na kurudi nyumbani

"Sisi kama taasisi inayojihusisha na michezo ya magari burudani hii inafundisha watoto kujua nidhamu ya vyombo moto hususani magari na kuwatoa katika michezo hatarishi " amesema Athumani

Na kwamba pia elimu ya usalama mashuleni na wamefanya ni kwa mara ya 3 hufanyika kila mwaka na tayari meshafikia shule saba kwa kushirikiana na kikosi cha usalama barabarani.

Aidha pamoja na kuwafikia watoto pia wamefanikiwa kuwafikia bodaboda zaidi ya 5000 kuwapatia elimu huku wakiwapatia elementi na vifaa vingine vya kufanyia shughuli zao bure kwa


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...