NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO

Takwimu zinaonyesha kuwa ajali nyingi za barabarani nchini  zinatokana na kutofuatwa kwa sheria za barabarani, madereva wasio na weledi na kitendo cha kutozingatiwa maswala ya kiusalama kwa vyombo vya usafirishaji ndio vyanzo vikuu vya ajali hizo.

Kwa mjibu wa ripoti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu( NBS) na  jeshi la Polisi, Katika kipindi cha Januari hadi Disemba mwaka 2023 jumla ya matukio 3,171,806 ya Usalama Barabarani yaliripotiwa katika vituo mbalimbali vya Polisi huku watu  Watu 1,645 wakiripotiwa kupoteza maisha na wengine 2,686 walijeruhiwa  ndani ya kipindi hicho.

Matukio hayo yameifanya kampuni ya Abood ( Abood Grop Company)   kuwalejesha darasani  madereva wake wanaofanya safari za kila siku kusafirisha kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine nchini, lengo likiwa ni kupunguza ajali zinazoepukika  hasa katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka.

Moles  masala ni msimamizi wa Mabasi kampuni ya Abood kizungumza na Waandishi wa Habari amesema lengo la kapuni hiyo ni kuwatoa madereva wake kuendesha magari kwa mazoea badala yake itakuwa inawajengea uwezo ili kuwawezesha madereva hao kufanya kazi  kwa weledi na kuzingatia sharia za usalama barabarani.

“Kampuni ya Abood haitomvulia dereva yeyote atakaye kiuka kanuni na sharia za usalama barabarani.” Amesema Moles

Kwa upande wake Afisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhiti na Usafiri Ardhini (LATRA) Mkoa wa Morogoro Bw.Andrew Mlacha amezitaka kapauni nyingine za mabasi kuiga mfano wa Abood kwa kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa madereva wao ili kuwakumbusha mambo mbalimbali yanaweza kusababisha ajali.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika la Afya duniani (WHO) inabainisha kwamba nchi nyingi ikiwemo Tanzania  zimeboresha sheria kama vile kuzuia mwendo kasi, ulevi na matumizi ya vifaa vya usalama kama matumizi ya mikanda, kofia za bodaboda yaani Helmet na hata viti maalumu kwa watoto.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...