BENKI ya Absa Tanzania imeibuka kidedea kwa kuibuka na ushindi wa kwanza wa Uandaaji Bora wa Taarifa za Fedha kwa Mwaka 2023 katika kitengo cha Mabenki yenye Ukubwa wa Kati wa tuzo za kila mwaka zinazoandaliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA).


Tuzo za mwaka 2023 zilishuhudia mchuano mkali ukihusisha washiriki 86 kutoka katika vitengo tofauti waliokidhi vigezo vilivyowekwa na NBAA ambapo washindi wake walikabidhiwa tuzo za na mgeni rasmi, Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Wizara ya Fedha, CPA. Benjamin Mashauri.

Akizungumza muda mfupi baada ya kupokea tuzo hiyo, Mdhibiti wa Masuala ya Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Muhsin Kaye alisema ushindi huo unaonesha ni kwa jinsi gani benki yao imebobea na kuwa na uzoefu, pamoja na watu wenye ujuzi wa kutosha katika uandaaji wa taarifa hizo.

“Ushindi huu ni ishara ya uwajibikaji sisi kama benki lakini pia uadilifu na uwazi katika uwasilishaji wa taarifa zetu, natoa ahadi kwa wateja wetu na kwa watanzania kuwa tutaendelea kujitahidi kuandaa taarifa sambamba na vigezo na kanuzi zinazohitajika na ni fahari kwetu sisi benki lakini ni fahari pia kwa wateja wetu wote.

“Ningependa kuishukuru Bodi ya NBAA kwa kuweka chachu ya uandaaji wa taarifa za kifedha kwa kuzingatia vigezo vilivyo sahihi kabisa, sisi kama benki tumefarijika kupata tuzo hii ikiwa ni muendelezo kwani tumeshapata tuzo hii miaka kadhaa iliyopita”, alisema Bw. Kaye.

Pamoja na hayo alisema, ushindi huo unaenda sambamba na lengo kuu la benki hiyo ambalo ni Kuiwezesha Afrika na Tanzania ya Kesho Pamoja, hatua moja baada ya nyingine, huku ikitiwa nguvu na ahadi ya chapa isemayo, ‘Story yako Ina Thamani.

“Sisi kama Absa Tanzania tunaamini ushindi huu utaendelea kuongeza ari na hamasa zaidi kwa benki yetu kufanya vizuri zaidi katika kuziwesha Story za mafanikio ya wateja wetu na watanzania kwa ujumla”, alisema Bw. Kaye.


Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Wizara ya Fedha, CPA. Benjamin Mashauri (wa pili kulia), akikabidhi tuzo ya mshindi wa kwanza wa Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Fedha katika kitengo cha Mabenki yenye Ukubwa wa Kati kwa Mwaka 2023 zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kwa Mdhibiti wa Masuala ya Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Muhsin Kaye katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA, CPA Prof. Sylvia Temu na Mkurugenzi Mtendaji NBAA, CPA. Pius Maneno.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA. Pius Maneno ( wa pili kushoto ) akimpongeza Mdhibiti wa Masuala ya Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Muhsin Kaye, mara baada ya benki hiyo kutangazwa mshindi wa kwanza kwanza wa Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Fedha katika kitengo cha Mabenki yenye Ukubwa wa Kati kwa Mwaka 2023 zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA, CPA Prof. Sylvia Temu na Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Wizara ya Fedha, CPA. Benjamin Mashauri.



Mdhibiti wa Masuala ya Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Muhsin Kaye (kulia), akipozi kwa picha ya kumbukumbu na pamoja na wawakilishi wa taasisi zilizoibuka na ushindi wa kwanza katika vitengo mbalimbali wakati wa hafla ya utoaji tuzo kwa washindi wa tuzo a Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Fedha zinazoandaiwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), jijini Dar es Salaam jana. Wengine katika picha ni mgei rasmi, Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Wizara ya Fedha, CPA. Benjamin Mashauri, Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA, CPA Prof. Sylvia Temu na Mkurugenzi Mtendaji NBAA, CPA. Pius Maneno.
Ofisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Bernard Tesha ( wa pili kushoto ), Mkuu wa Mikakati na Bidhaa za Wateja Binafsi, Bw. Heristraton Genesis ( kushoto), Mdhibiti wa Masuala ya Fedha, Muhsini Kaye na Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi, wakionesha tuzo ya Uwasilishaji Bora wa Taarifa za Fedha katika kitengo cha Mabenki yenye Ukubwa wa Kati kwa Mwaka 2023 zinazotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), muda mfupi baada ya kukabidhiwa jijini Dar es Salaam jana.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...