Ujumbe wa Benki Kikuu imelidhishwa na utekelezaji wa Mradi Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) unaotekelezwa Chuo Kikuu Mzumbe baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo mapya ya Taaluma, lengo likiwa ni kuboresha miundombinu ya kufundishia.

Akizungumza katika ziara hiyo ya siku moja ya Ujumbe kutoka Benki Kikuu ulioambatana na Wataalam kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha amesema mradi huo wa ujenzi wa majengo mapya ya Taaluma yanaghalimu shilingi milioni 13.2 fedha kutoka Benki ya Dunia.

Kiongozi timu ya Benki ya Dunia Prof. Roberta Malee  amekitaka Chuo Kikuu Mzumbe  kuzingatia viwango vya ubora katika ujenzi wa majengo hayo ili kunufaisha kizazi cha sasa na badaye huku akiipongeza menejimenti kwa usimamizi mnzuri wa mradi  huo kwa hatoa uliofikia.

Dkt. Kennedy Hosea, mratibu wa mradi wa HEET nchini Tanzania, amesisitiza umuhimu wa kukamilisha mradi huo  kwa wakati, akisema kuwa ni hatua muhimu katika kuboresha mfumo wa elimu ya juu nchini. “Mradi huu unalenga kutoa fursa za kujifunza zinazokidhi mahitaji ya soko la ajira”. Amesema

Msanifu wa majengo Bw. Fadhili Msemo, amesema majengo haya yatakuwa na madarasa, maabara za kisasa, na maeneo ya kufanya tafiti za TEHAMA huku yakitarajiwa kuongeza chachu ya maendeleo ya kitaaluma na kiteknolojia kwa wanafunzi na wahadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe.

Kampuni ya Shanxi Construction Investment Group kutoka China ndio inayoongoza ujenzi wa majengo hayo, baada ya kusaini mkataba wa  ujenzi wa miezi 18  mwezi Agosti mwaka huu.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...