-Wasema wanarudisha faida kwa jamii, na waishukuru serikali kuingiza pikipiki

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

Umoja wa Maafisa Usafirishaji wa Bodaboda Mabibo Mwisho (BMM) umesema kuwa unaishukuru serikali katika utashi wake wa kuingiza Pikipiki ambazo zimekuwa msaada wa vijana kujiajiri.

Vijana katika kujiajiri huko ni fursa nyingine katika kurudisha mafanikio kwa watu wengine ambao watajiajiri.

Akizungumza na Michuzi Media Mabibo Mwisho Mwenyekiti wa (BMM) Hamis Mwela amesema wakati sasa umefika kusaidia wengine ambao ni mabondia kuwafadhili katika kazi hiyo.

Amesema katika utaratibu wao wa kuchangishana wameweza kuwa na fedha ya kuwafadhili mabondia wawili kuingia nao mikataba.

Amesema kuwa mabondia hao watasimamia katika mazoezi yao pamoja na masuala mengine katika maisha yanayoendelea ya kila siku.

Mwela amesema kuwa katika umoja wao kumekuwa na mwitikio katika udhamini huo kwani unatokana na michango yao ya kila siku.

Aidha amesema kuwa watashirikiana na mabindia hao katika mapambano ambapo mapromota wakiwahitaji katika mapambano wawasiliane na BMM.

Hata hivyo amesema kuwa wananchokitoa kwa sasa ni kuwainua vijana wenzao katika ubondia na wao waje kurudisha kwa makundi mengine.

Bondia Paul Anastaz (Magesa)mwenye uzito kilo 60 wa amesema kuwa anashukuru udhamini wa BMM na kuahidi kufanya kazi ya ubondia kwa ufanisi katika mapambano akayokutana nayo.

Kwa upande wa Rashid Hemed Rashid amesema yuko tayari kwa kazi yeyote ya ubondia kutokana na kupata ufadhamini na ufadhili kwa BMM.

Amesema katika kipindi kirefu alikuwa hajapata mdhamini na mfadhili na kufanya kazi yake kuwa ngumu ikiwemo kulipa gharama za mazoezi.
 

Bondia Paul Anastaz (Magesa) akijifua na mazoezi baada kupata ufadhili wa BMM,Jijinj Dar es Salaam.
 

 Paul Anastaz na Hemed Rashid wakizichapa katika mazoezi ya ngumi mara baada ya kupata udhamini wa BMM jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa BMM Hamis Mwela akiazungumza kuhusiana na udhamini wao kwa mabondia wa ngumi ikiwa ni kurudisha mafanikio yao kwa jamii,jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...