Tamasha kubwa na la mwisho la Coca-Cola Food Festival linatarajiwa kufanyika tarehe 23 Novemba katika kiwanja cha St. Laurent kilichopo Kawe jijini Dar es Salaam. Tukio hili litaleta pamoja wapenda vyakula na burudani katika siku ya kufurahia vyakula mbalimbali na vya kipekee huku vikiambatana na burudani za muziki wa kisasa na kitamaduni.
Zaidi ya Mama Lishe na Baba Lishe 20 ambao walipata fursa ya kuwa kwenye kampeni yay a kila wiki ya Kitaa Food Fest, wataungana na wapishi maarufu na wabunifu wa maudhui ya vyakula kutoka Tanzania na Afrika Mashariki. Wapishi hao maarufu ni pamoja na Diko na Monalisa, wa hapa Tanzania na Dennis Ombachi, mchezaji wa Rugby kutoka Kenya anayejulikana kama ‘The Roaming Chef’.
Washiriki watapata fursa ya kuchunguza urithi wa vyakula vya Tanzania, vilivyopikwa kwa ubunifu na umahiri.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, Fatma Mnaro, Mkurugenzi wa Mauzo na Biashara Coca-Cola Kwanza Ltd alisema, “Tamasha hili kubwa linaashiria kilele cha Kampeni ya Coca-Cola Food Fest Tanzania, ambayo imekuwa na mfululizo wa mizunguko zaidi ya 80 iliyofanyika katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam na miji mingine mikubwa tangu kuzinduliwa kwa tamasha hili katikati ya Septemba. Shughuli hizi zimewapa wauzaji na wapishi wa ndani jukwaa la kuonesha vipaji vyao vya upishi huku zikihamasisha ushiriki na kuongeza mauzo.”
Kwa upande wake Meneja Mwandamizi wa Masoko wa Kampuni ya Coca-Cola, Kabula Nshimo alisema kuwa, Tamasha hilo kubwa la Coca-Cola Food Festival litakuwa na ladha mbalimbali za vyakula vya kitamaduni na yote ni katika kusherehekea ubunifu na kuwaleta watu pamoja kupitia uzoefu wa pamoja. “Siku ya tarehe 23 Novemba itakua ni siku ya shamra shamra, kula na kusaza katika kusheherekea utamaduni vya vyakula vya kitanzania.
Tukio hili litaambatana na burudani mbali mbali ya muziki kutoka kwa Ma Dj na wasanii wa Tanzania pia linaendana na kampeni ya kimataifa ya Coca-Cola ya “A Recipe for Magic,” ambayo inasherehekea nguvu ya chakula cha pamoja katika kuwaunganisha watu.
Tiketi za kiingilio za Tamasha hili zitauzwa kwa TZS 15,000/= kwa kila mtu, ambapo inajumuisha chakula pamoja na kinywaji kutoka Coca-Cola. Washiriki wanaweza kununua tiketi kwenye lango la kuingilia au kununua mapema kupitia programu ya Nilipe kwa TZS 10,000/= hadi tarehe 22 Novemba 2024 (bei ya awali).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...