Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mussa Kilakala ameupongeza Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kutoa elimu ya ufuatiliaji matukio ya moto kwa kutumia mfumo wa satelaiti kwa wahifadhi wa TFS, ambapo mafunzo hayo yanatoa mwanga katika kukabiliana na majanga ya moto katika hifadhi ya misitu ya asili na mashamba ya miti.
Mafunzo hayo ya siku tatu yametolewa kwa wahifadhi wa TFS 30 kutoka katika mashamba ya miti na hifadhi za misitu ya mazingira asilia kutoka TFS kanda ya mashariki inayojumuisha mikoa ya Pwani, Morogoro na Dar es salaam, yaliyofanyika mjini Morogoro. Mafunzo hayo yanalenga kupunguza visumbufu vya rasilimali za misitu ukiwemo moto ambao mara kadhaa umekuwa ukizuka katika maeneo ya misitu.
Akifunga mafunzo hayo Mkuu wa wilaya ya Morogoro Mhe, Kilakala amesema kuwa mafunzo haya yataongeza ufanisi katika kufuatiliji matukio ya moto katika misitu ya hifadhi na mashamba ya miti ambayo imekuwa na faida kubwa katika utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji.
Mhifadhi mkuu ugani na uenezi TFS kanda ya mashariki Shaaban Kiulah amesema kuwa TFS itaendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ambayo inalenga kuongeza chachu katika kudhibiti matukio ya moto katika misitu yote hapa nchini.
Aidha Kiulah amewataka washiriki wa mafuzo hayo kuhakikisha wanatumia elimu walioipata katika kudhibiti matukio ya moto katika vituo vya kazi wanayotoka.
Eimu hii itapunguza matukio ya moto katika maeneo yetu ya hifadhi kwani taarifa wahifadhi watapata kwa haraka kupitia mifumo wa setilaiti na kuchukua hatua za haraka kuudhibiti moto huo kabla ya kuleta madhara ndani ya misitu ya hifadhi.
Kwa upande wake Afisa uhifadhi TFS Elin Jasto amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kupata mbinu mpya ambazo zitasaidia kupunguza madhala yatokanayo na moto ambapo amesema kuwa awali walikuwa wanatumia wananchi katika kupata taarifa likini baada ya mafunzo hayo wataweza kutambua viashiria moto jambo litakalosaidia kudhibiti mapema kabla haujaleta madhara.
Mhifadhi Rogers Nyinondi ni mkufunzi wa Mafunzo hayo kutoka kitengo cha kupambana na moto wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) amesema mafunzo hayo ni sehemu ya ya mpango wa muda mrefu wa kukabiliana na matukio ya moto lengo kubwa ni kuhakikisha matukio ya moto yanathibitiwa pale yanapotokea pia kufuatilia viashiria vya moto kabla haujatokea na kuchukua tahadhari
Washriki wamepata fursa ya kujifunza mambo mblimbali ikiwemo namna ya kutambua viashiria vya matukio ya moto hifadhini kupitia mifumo ya setelaiti kabla haujatokea na kutengeneza mfumo wa kupata ujumbe mfupi kupitia simu ya mkononi ambao unatoa taarifa ya tukio la moto limetokea muda gani na wapi hivyo itawasaidia wahifadhi kuona matukio ya moto mapema zaidi ukilinganisha na awali.
Home
HABARI
DC KILAKALA AITAKA TFS KUTOA ELIMU UFUATILIAJI MATUKIO YA MOTO KWA MIFUMO YA SETELAITI KWA TAASISI ZA UMMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...