Na Humphrey Shao, Michuzi Tv

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, ameipongeza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa utekelezaji wa maagizo ya serikali ya kuhakikisha utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa vijana, wanawake na wenye ulemavu unafanyika kwa kuzingatia utoaji wa elimu kabla ya kutoa mikopo hiyo.

Mpogolo ametoa shukrani hizo wakati wa Kongamano la Uelimishaji na Uhamasishaji Jamii Juu ya Uwepo wa Mikopo kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu Sambamba na Matumizi ya Nishati Safi linalofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam tarehe 11 Novemba 2024, katika Uwanja wa Mnazi Mmoja, ambapo alihudhuria kama mgeni rasmi.

"Nikupongeze Mkurugenzi Mabelya na timu yako kwa kuzunguka kwenye kata zote 36 na mitaa 159 ya Ilala ili kutoa mafunzo kwa wajasiriamali. Leo hii tunashuhudia maonesho na mafunzo ya pamoja kwa wale ambao hawakupata nafasi ya kuhudhuria katika maeneo mengine," amesema Mpogolo.

Mpogolo amesema kwamba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameruhusu halmashauri hiyo kutoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 14 kwa vikundi vya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu, hatua inayolenga kuwainua kiuchumi na kuboresha maisha ya wananchi wa Dar es Salaam.

"Halmashauri yetu ya Ilala ni ya kipekee kwa kutoa mikopo mikubwa kuliko halmashauri zote nchini. Tunatoa mikopo kwa wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao ndani ya Ilala, bila kujali wanakotoka, mradi wanachangia uchumi wa eneo hili," amesisitiza Mpogolo.













Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...