Na Oscar Assenga, MUHEZA.

MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Zainab Abdallah Issa amewataka wananchi wilayani humo kutimiza haki yao ya msingi kuchagua viongozi wanaowataka kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaofanyika leo hapa nchini.

DC Zainab aliyasema hayo mara baada ya kushiriki zoezi la kupiga kura katika Ofisi ya Mtendaji Kata Mbaramo wilayani humo huku akisisitiza kwamba ulinzi na usalama umeimarishwa kwenye maeneo yote ya kupigia kura.

Alisema zoezi la kupiga kura ni haki ya kila mwananchi ambaye alijiandikisha hivyo uwepo wa ulinzi na usalama kwenye vituo vya kupigia kura unawapa nafasi wananchi kutimiza haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wanaowataka.

Alisema kwamba ni muhimu wananchi kujitokeza mapema kupiga kura kutokana na kuwa zoezi hilo ni la muda mfupi wanapofika kwenye vituo wana hakiki majina na kuingia kwenye mchakato wa kupiga kura

“Nitoe wito kwa wana Muheza na Watanzania kujitokeza kwa wingi tutimize haki yetu ya msingi kuwachagua viongozi ambao tunawakata kwa maslahi ya maendeleo ya maeneo yetu kwa miaka mitano ijayo”Alisema

“Niwaombe leo ni siku ya mapumziko huna sababu ya kusubiri mpaka saa 10 jioni twendeni tukapige kura hali ya usalama kila mahali imeimarishwa na mungu atatujalia mpaka tutakapofunga tutafunga kwa usalama”Alisema DC Zainab.

Hata hivyo aliwapongeza wananchi wa wilaya hiyo waliojitokeza kwa wingi kwenye zoezi la uandikishaji huku akieleza kwamba katika zoezi hilo la upigaji kura wataendelee kuhamasishana.
“Pale ulipojiandikisha ndio utakapopiga kura imani yangu wana Muheza 187,000 kama walivyojiandikisha tutapiga kura na tutahakikisha zoezi linakamilika salama.

Awali akizungumza mara baada ya kupiga kura kwenye kituo hicho cha kupigia kura Mkazi wa Mbaramo wilayani Muheza Martha Joseph alisema wanamshukuru mungu wameanza kupiga kura saa mbili asubuhi na mpaka sasa zoezi linaendelea vizuri na hivyo wanaamini litamalizika salama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...