Na Mwamvua Mwinyi Novemba 20,2024
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha ,Dkt.Rogers Jacob Shemwelekwa amekutana na Wamiliki na Wafanyabiashara ya mafuta kuwakumbusha kuwa wazalendo kwa Taifa,kufanyabiashara kihalali na kulipa Kodi ya Serikali kwa wakati.
"Nawasihi sana,nipeni ushirikiano ili sote tukishirikiana tupate Mapato yatakayo hudumia wananchi. Tukiungana kukusanya Mapato,tunakwenda kuibadili Kibaha Kimaendeleo"amesema Dkt.Shemwelekwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe.Nickson Simon John ametoa vyeti Maalum kwa kampuni ya Admire na National oil kutambua wepesi wao wa kulipa Kodi kwa wakati.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...