Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Shahada ya Udaktari ya Heshima (PhD) katika uongozi, leo tarehe 24 Novemba 2024, kwenye mahafali ya 23 ya Chuo Kikuu cha Mzumbe, yaliyifanyika Kampasi Kuu ya Morogoro.

Shahada hiyo aliyotunukiwa Mhe. Rais Dkt. Samia, imetokana na umahiri na uwezo aliouonesha kwenye uongozi katika nafasi mbalimbali alizotumikia taifa, kupitia Chama na Serikali na nje ya hapo.

Pia Dkt. Samia leo ni mgeni maalum kwenye mahafali hayo yanayofanyika katika Viwanja vya Maekani.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...