Na Nasra Ismail, Geita
Halmashauri ya Wilaya ya Geita imeongoza kati ya Halmashauri Sita za Mkoa wa Geita katika Matokeo ya Mbio za Mwenge wa Uhuru zilizofanyika Oktoba 5, 2024.
Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 zilianza Mkoani Kilimanjaro Aprili 2, 2024 ambapo Mhe Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa (MB) alizindua mbio hizo na kuhitimishwa Oktoba 14, 2024 jijini Mwanza na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Mratibu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Halmashauri ya Wilaya ya Geita Ndg Alex Herman ameelezea furaha aliyo nayo kwa matokeo hayo na kusema kazi haikuwa ndogo.
“Sikutegemea kwa kweli kutokana na misukosuko na changamoto nyingi sana wakati wa maandalizi hayo ila Mwenyezi Mungu amewezesha na hatimaye tumekuwa washindi,” amesema Alex.
Aidha Mratibu huyo ametoa shukrani kwa kamati zote zilizowezesha mapokezi ya mbio za mwenge wa uhuru 2024.”Kipekee sana nipende kuishukuru kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya Mh. Hashim Komba, Mkurugenzi Ndg.Karia Rajabu Magaro,viongozi wa chama na dini, wakuu wa idara na vitengo, Taasisi mbalimbali ikiwepo Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini TARURA na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Geita (GEUWASA), wadau mbalimbali kwa namna walivyotoa michango yao pamoja na wananchi wote kwa jitihada na kuonesha ushirikiano kipindi chote cha maandalizi hadi tulipokabidhi Mwenge wa Uhuru Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema OKtoba 6,2024.” ameongeza Alex.
Pamoja na kuwa ya kwanza Kimkoa, Halmashauri ya Wilaya ya Geita imeshika nafasi ya 6 kwa kanda yenye halmashauri 45 na kushika nafasi ya 17 kitaifa kati ya Halmashauri 195 zilizokimbiza Mwenge wa Uhuru 2024.
Mwenge wa Uhuru ni chombo kilichoasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1961 ikiwa ni tunu na ishara ya kuwepo kwa Taifa huru la Tanganyika.
Mbio za Mwenge wa Uhuru zilianza rasmi mwaka 1964 baada ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwenge wa uhuru umekuwa kichocheo kikubwa katika kuimarisha uhuru wa Taifa la Tanzania,umoja wa kitaifa, kudumisha amani, kulinda Muungano na kuhamasisha maendeleo ndani na nje ya taifa la Tanzania.
Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2024 imesema “Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu”

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...