Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Eastern Star kwa ushirikiano wa Kampuni ya The Global CEO Institute imetoa Tuzo za watendaji wakuu bora 100 kwa mwaka 2024 huku Waziri Nchi Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Sharif Ali Sharif akipongeza utolewaji wa tuzo.
Pia ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa Vijana wa kitanzania kuhakikisha wanabuni miradi inayoendana na sera za uwekezaji ili wawe sehemu ya kujenga uchumi wa nchi yao.
Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo za Watendaji wakuu Bora 100 wa mwaka pamoja na wakuu wa taasisi mbalimbali zikiwemo kampuni zilizofanya vizuri mwaka 2024 amesisitiza umuhimu wa vijana kuwa sehemu ya kujenga uchumi kwa vitendo.
Waziri Ali Sharif ameongeza kwamba vijana wana nafasi ya kufanya kampuni zao kutambulika katika soko la ndani na nje iwapo watatumia vyema mazingira mazuri ya uwekezaji ndani ya nchi yao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Eastern Star Deogratius Kilawe ambaye ndie muandaaji wa tuzo hizo kwa ushirikiano wa Kampuni ya The Global CEO Institute,amesema dhumuni la kuandaa tuzo hizo ni kusherehekea uongozi bora, kukuza uvumbuzi, na kuhamasisha kizazi kijacho cha watendaji.
Pia ni katika kukuza na kuweka viwango pamoja na kuleta mabadiliko chanya na matokeo ya kudumu katika tasnia na jumuiya tunazohudumia huku akieleza kuwa ugawaji wa tuzo hizo umezingatia ubora wa kazi zilizofanywa na washiriki.
Kwa baadhi ya washindi wameeleza kuwa tuzo hizo zinatia chachu kwa Kampuni za Kitanzania kuendelea kufanya vizuri mwaka hadi mwaka kwa kubuni bidhaa zinazokidhi mahitaji ya soko la Kimataifa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...