METL Group imezindua rasmi Kampeni ya Malkia mwenye Chombo, mradi wa kipekee unaolenga kuwawezesha wanawake kwa kuwapatia Bajaj mpya kwa mkopo wa masharti nafuu. Mpango huu unaendeleza dhamira ya METL ya kushiriki katika maendeleo ya jamii na kubadilisha maisha ya wengi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya City Blue jijini Dar Es Salaam, Bi. Fatema Dewji, Mkurugenzi wa Masoko wa METL na Mwenyekiti wa Bodi ya MO FINANCE, alisema, “Malkia mwenye Chombo ni mwendelezo wa desturi ya METL ya kuinua jamii. Tuna furaha kuona familia nyingi sana zimewezeshwa kupitia miradi yetu, na kampeni hii ni hatua nyingine muhimu ya kuinua kundi kubwa zaidi.”

Kwa upande mwingine, Bw. Soumya Das, Makamu wa Rais wa Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini - Bajaj Auto Ltd India, alisifu kampeni hiyo na kubainisha kuwa mpango huu wa kutoa nafasi kwa wanawake unafuatwa na kampuni ya Bajaj pia. “Sisi kutoka Bajaj Auto tunafurahi kwamba mshirika wetu mashuhuri wa usambazaji, MeTL Group, leo anazindua mpango wa ‘Malkia Mwenye Chombo.’ Mpango huu unalingana na juhudi zetu kutoka Bajaj Auto za kusaidia wafanyakazi wetu kufanikiwa katika taaluma zao. Katika viwanda vyetu, tuna mistari ya uzalishaji inayojumuisha wanawake pekee wakitengeneza pikipiki kubwa na magari ya umeme.”

Aidha, Bw. Ashish Joshi, Mtendaji Mkuu wa kanda wa MeTL, alisisitiza upekee wa mpango huu, akionyesha jinsi juhudi za pamoja za MeTL, Bajaj na MO Finance zitakavyowezesha wanawake na kukuza uhuru wao wa kifedha.

“Chini ya mpango huu, MeTL Bajaj itazingatia uwezeshaji wa vitendo kwa kutoa mafunzo ya kuendesha Bajaj RE 4S, kutoa elimu, kuhusu sheria za barabarani, na kuwasaidia washiriki kupata leseni za kuendesha Bajaj kutoka kwa mamlaka husika. Hii inahakikisha kuwa wanawake wanakuwa na ujuzi na sifa zinazohitajika kwa ajili ya usafiri na ujasiriamali.”

Hafla ya uzinduzi inatoa fursa kwa wanawake kufanikisha uhuru wa kifedha na kujenga maisha endelevu kwa ajili yao na wapendwa wao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...