Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Vijana Taifa wa Chama cha Mapinduz(CCM),Juliana Didas Masaburi amesema katika kushika dola uchaguzi wa Serikali za Mitaa ndio uchagizi wa kuangalia kutokufanyia masihara.

Hivyo ni wajibubwa wanachama wote wa CCM kuhakikisha mwaka huu wamejipanga kupiga kura kuhakikisha wanashinda kwa kishindo.

Massaburi ameyasema hayo Novemba 23,2024 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mpiji darajani kata ya kibosha ikiwa ni muendelezo wa mikutano ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji unaotarajia kufanyika Novemba 27 mwaka.

Alisema uchaguzi wa serikali za mtaa unaangaliwa sana kwa kuwa ni moja ya njia ya kuja kumsaidia rais katika utendaji wake wa hapo baadae, hivyo amewataka wananchi kufanya maamuzi sahihi wakati wa kupiga kura.

"Tunarajia mwaka huu katika vitongoji vya mapinga mtawapigia kura zote wagombea 8 wa CCm ili baadae waweze kuongea kauli moja ni vyema kura zote ziwe za CCM ili kuibuke ushindi wa kishindo" alisema

Alisisitiza kwa kuona mliweza kumteuwa mgombea kijana ndio maana tumeweza kufika ili kuweza kumuombea kura za ndio mgombea mliomteuwa ili naadae mpate wa kuwasemea.

Aliongezea kuwa mnatambua sasa hivi mambo mengi ni 'connection' mmefanya mema kumchagua mgombea kijana naamini atawaunganisha ilikuweza kufika mbali,

"Basi kwa desturi ya kwetu huwa tunatumia kupiga magoti kwa ajili ya kuomba na leo nitapiha magoti kwa ajili ya kuombea kura za ndio wagombea wote wa kata ya mapinga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...