Mkutano wa 34 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango umeanza leo tarehe 04 Novemba 2024 jijini Arusha.

Mkutano unaotarajiwa kufanyika kwa siku tano kuanzia 4-8 Novemba 2024 umeanza katika Ngazi ya Wataalam na na baadaye utafuatiwa na Ngazi ya Makatibu Wakuu, watakao kutana tarehe 7 Novemba 2024 na kuhitimishwa na Mkutano Ngazi ya Mawaziri ukaofanyika tarehe 8 Novemba 2024.

Mkutano huo katika Ngazi ya Wataalam pamoja na mambo mengine utapokea na kujadili mapendekezo na taarifa mbalimbali za Jumuiya ikiwemo: maendeleo ya utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya, kuhuisha masuala ya kuondoa vikwazo visivyokuwa vya kibiashara (NTBS) katika Jumuiya, kujadili taarifa ya maendeleo ya eneo huru la biashara la soko la utatu la COMESAS-EAC-SADC na kujadili taarifa ya maendeleo ya Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AFCFTA).

Masuala mengine yatakayo jadiliwa ni pamoja na maeneo ya vipaombele kwa mwaka wa fedha 2025/2026, randama ya taarifa ya nusu mwaka ya Mkakati wa 6 wa Maendeleo ya Jumuiya, taarifa ya agenda ya pili ya utafiti katika Jumuiya, taariafa ya utekelezaji wa maagizo ya mkutano wa kawaida wa Baraza la 45 kuhusu kufanya maboresho ya nembo za Jumuiya na taarifa ya maandalizi ya maadhimisho ya miaka 25 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Akifungua mkutano huo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Bw. Aime Uwase Mkurugenzi Mipango wa Sekretarieti ya Jumuiya hiyo amehimiza kuhusu umuhimu wa mkutano huo katika kutathimini, kupanga na kusimamia utekelezaji na wa sera na mipango iliyowekwa kwa maendeleo ya Jumuiya.

Mkutano huo unaofanyika kwa njia mseto (Video na ana kwa ana) umehudhuriwa na nchi zote Wanachama wa Jumuiya, huku ujumbe wa Tanzania ukijumuisha; Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Mhandisi Abdillah Mataka, Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama Bi. Mwanamridu Amity Jumaa, Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathimini Bw. Haji Janabi, Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. Justin Kisoka, ambaye pia ni kiongozi wa ujumbe huo, wote kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Mkurugenzi wa Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Justin Kisoka akichangia kwenye Mkutano 34 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango unaofanyika jijini Arusha.
Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Mhandisi Abdillah Mataka akichangia kwenye Mkutano wa 34 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango unaofanyika jijini Arusha.

Sehemu ya ujumbe kutoka Jamhuri ya Burundi ukifuatilia Mkutano wa 34 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango unaofanyika jijini Arusha.

Mkutano ukiendelea

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...