Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
MMILIKI wa Gorofa la Kariakoo lililoanguka hivi karibuni na kupelekea vifo vya watu 31 na kuacha wengine majeruhi Leondela Mdete na wenzake wawili, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 31 ya kuua bila kukusudia.
Mbali na Mdete, washtakiwa wengine ni Zenabu Islam 61) na Ashour Awadh Ashou (38)
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Adolf Lema akisaidiana na Grace Mwanga na Erick Kamala imedai washtakiwa walitenda makosa hayo Novemba 16, 2024 katika mtaa wa Mchikichi na Congo eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Godfrey Mhina inadaiwa siku ya tukio isivyo halali, washtakiwa walishindwa kutimiza majukumu yao na kusabashisha vifo vya Said Juma, Hussein Njou, Prosper Mwasanjobe, Shadrack Mshingo, Godfrey Sanga, Neema Sanga, Elizabeth Mbaruku, Hilary Minja, Abdul Sululu, Chatherine Mbilinyi na wengine 21
Hata hivyo washtakiwa wamekana kutenda kosa hilo na mshtakiwa Mdete ameachiwa huru kwa dhamana wakati mshtakiwa Islam na Ashour wakirudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambayo yaliwataka kuwa na
wadhamini wawili kila mmoja wenye barua za utambulisho, kitambulisho cha Taifa na walitakiwa kusaini bondi ya Shilingi Milioni Tano kwa kila mmoja.
Kesi imeahirishwa hadi Desemba 12, mwaka huu 2024
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...