NA DENIS MLOWE, MAFINGA 


MWENYEKITI wa Ccm Mkoa wa Iringa, Daud Yassin Mlowe, na Mke wake Blandina Paul wameazimisha miaka 45 ya ndoa katika misa iliyofanyika katika Kanisa la EAGT Jerusalem Temple lililoko Mjini Mafinga na kuongozwa na Askofu Brown Mwakipesile.


Wageni wengine maarufu waliohudhuria maadhimisho hayo pamoja na wafanyabiashara wakubwa wilaya ya Mufindi wakiongozwa na Chesco Ng'umbi maarufu kwa jina la Makambako mmiliki wa vituo vya mafuta vya Cf Ng'umbi , mwenezi wa ccm wilaya Mufindi, Dickson Lutevele 'Villa' na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Mufindi na madiwani wa kata mbalimbali wakiambatana na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Mafinga.


Akizungumza katika misa ya shukrani ya kuadhimisha miaka 45 ya ndoa Askofu Brown Mwakipesile alisema kuwa vijana wa nyakati hizi wanaoa kwa tamaa bila kumshirikisha Mungu hivyo wametakiwa kuwa na chaguzi sahihi ya kuoa au kuolewa badala ya kufata maumbo pesa na mali.


Aliongeza kuwa kama viongozi wa dini zote wanajambo la kufanya kuhakikisha jamii inapata elimu kuhusu masuala ya ndoa kabla na baada ya ndoa.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti waalikwa baadhi walisema kuwa ni mfano wa kuigwa kwa baadhi yetu katika kuweza kutimiza miaka 45 ya ndoa kitu ambacho si mchezo.


Chesco Ng'umbi alisema kuwa jamii ya sasa imekuwa ikiingia kwenye ndoa kwa kurupuka hali ambayo wengi wao wanashindwa kumudu mikimiki iliyomo ndani ya ndoa.


Alisema kuwa ufike wakati vijana kabla ya kuingia kwenye ndoa wajipange vyema na kuwa chaguzi sahihi na kumfanya Mungu ndio mwongozo wa ndoa zao.


"Ujue miaka 45 ya ndoa si mchezo inawezekana wazee wetu hawa Waliingia kwenye ndoa wakiwa wamejipanga vyema hali ambayo imefanya waishi katika changamoto zote za maisha kitu ambacho vijana wa sasa hawawezi kutokana na kukurupuka"


Naye Jasmin Chesco alisema ifike wakati vijana kuepukana na tamaa za kimwili pale ambapo wanahitaji kujenga mahusiano kwani tamaa ni chanzo cha ndoa nyingi kuvunjika.


Sisi kama vijana tunahitaji kuiga mazuri ambayo yameonyeshwa kwenye ndoa ya mzee Yassin na Mke wake kwani kukaa miaka 45 ya ndoa kuna mengi wamepitia ila kwa kumtanguliza Mungu na kuepuka tamaa mbalimbali ambazo ni hatarishi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...