TAASISI,Mashirika yanayojihusisha na Vijana watakiwa kuwatengenezea mifumo Vijana hao kuwa wenye tija na Msaada kwa Taifa katika umri huo mdogo ili kukuza chachu ya Maendeleo.

Akizungumza hayo Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Jumanne Sagini wakati wa Maadhimisho ya Kumbukizi ya Miaka 100 ya Kuzaliwa kwa Sheikh Kaluta Amir Abeid na Miaka 60 ya Kifo chake sanjari na Kuzinduliwa Kwa Taasisi yake iliyofanyika Jijini Dar es ,Jumanne amesema Hayati Kaluta aliweza Kufanya Mapinduzi ya Kimaendeleo akiwa na umri mdogo zaidi Kushika Nyazifa mbalimbali na kuhakikisha baadhi ya Maeneo anaacha Alama ambayo Leo hii ni Kumbukumbu kwa Vizazi vilivyopo na vijavyo.

Hata hivyo ameongeza kuwa Hayati alikuwa na mchango katika kukuza Lugha ya Kiswahili na kuhakikisha Kiswahili inaendelea kuenea ni kupitia kitabu cha kanuni za ushairi na kitabu cha Diwani ya Amri.

Aidha Sagini amesema kuwa atahakikisha Wizara yake inatunga Sheria Kwa Lugha ya Kiswahili ili ziweze kuwasaidia Wananchi na Kuwafikia Maeneo mbalimbali nchini.

"Nitahakikisha Wizara ya Katiba na sheria tunaandaa Sheria kwa Lugha ya Kiswahili ili kuwaenzi Waasisi waliopigania Lugha hii inafika duniani kote,bali pia Kurahisisha Mawasiliano baina ya watu ambao hawawezi kutumia lugha ya Kiingereza ambapo kwa sasa watu wengi wanapitia kadhia ya kusoma mikataba na sheria kwa Lugha ambayo kwao imekuwa changamoto. "

Sagini ametoa wito pia kwa Baraza la Kiswahili Taifa (BAKITA ) na Wadau Wengine wa Lugha ya Kiswahili kuendeleza kuandaa Makongamano ambayo Kimsingi ina lengo la kukuza lugha ya Kiswahili .

Pia ametoa rai Kwa Vijana kujifunza kutoa mchango kwa taifa huku akizikumbusha taasisi zinazohihusisha na Vijana kuweka mifumo rafiki ili waweze kuwaandaa Vijana na Kuwawezesha Kulitumikia taifa mapema .

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo Hamis Mwinjuma amesisitiza umuhimu wa tukio la Kuwaenzi Mashujaa , akieleza kuwa linaangazia mchango wa Sheikh Kaluta Amri Abeid katika kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili, hasa katika nyanja za sarufi, fasihi, na utangazaji wa Kiswahili duniani.

"Mhe. Mwinjuma amesema, 'Serikali ya Tanzania itaendelea kuunga mkono juhudi za kukuza Kiswahili, ikiwa ni pamoja na kuenzi kazi za mashujaa kama Sheikh Kaluta, na kuhakikisha lugha hii inazidi kuwa nyenzo ya maendeleo na utambulisho wetu kama Taifa.'"

Aidha Kwa Upande wake Muwakilishi Taasisi ya Sheikh Kaluta Amri Abeid, Amiri Abeid Kaluta ametoa Pongezi kwa Viongozi, Taasisi,Makampuni na Mashirika ambayo yamefanikisha Kumbukizi hiyo .


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...