Na Karama Kenyunko Michuzi Tv 

MKURUGENZI Mwanzilishi wa Kampuni ya Vanilla International Ltd, Simon Mkondya (40) maarufu kwa jina la  Dkt. Manguruwe  na mwenzake wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka 28.

Katika kesi hiyo, Mkondya na Mwenzake Rweyemamu John ambaye ni Mkaguzi wa kiwanda hicho wanakabiliwa na mashtaka 19 ya upatu na mashtaka tisa ya kutakatisha viwanja vilivyopo huko Njombe eneo la Idunda.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Job Mrema mbele ya Hakimu Mkazi Aaron Lyamuya inadai washtakiwa walitenda kosa hilo kati ya January Mosi 2020 na Desemba 2023 jijini Dar es Salaam. 

Inadaiwa  katika kipindi hicho  Mkondya akiwa kama Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanilla pamoja na mkaguzi wake huyo walifanya biashara ya upatu kwa kuwaahidi watu kuwa ukitoa kiasi chochote cha pesa utapata faida mara tatu ya kiasi ulichotoa.

 Inadaiwa washitakiwa walijipatia jumla ya Sh Milioni 92.2 kutoka kwa watu kumi na tisa tofauti ikiwa kila mmoja alimpatia kiasi chake cha fedha akimuahidi kuwa fedha hizo zingezaa mara tatu ya zile alizotoa.

Katika mashtaka tisa ya utakatishaji mshtakiwa Mkondya peke yake anadaiwa katika kipindi hicho hicho, akiwa ndani ya Mkoa wa Dar es salaam  alijipatia jumla ya viwanja tisa vitalu namba Ab vilivyopo eneo la Idunda Mkoani Njombe huku akijua kuwa viwanja hivyo ni mazalia ya kosa  tangulizi la upatu.

Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida husikilizwa mahakama Kuu ama kwa kupewa kibali kutoka kwa mkurugenzi wa mashtaka DPP.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika. 

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 19,2024 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa. Mshtakiwa amerudishwa rumande.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...