Benki ya Standard Chartered imepanda miti 2000 ya matunda na kivuli katika Shule ya Msingi Kigongoni iliyopo kata ya Magomeni Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani ikiwa ni mwendelezo wa kampeni waliyoianzisha miaka mitatu iliyopita kuunga mkono juhudi za serikali za utunzaji mazingira.

Akizungumza shuleni hapo Ofisa Mkuu Mwendeshaji na mambo ya Teknolojia wa benki hiyo Christopher Vuhahula aliwahimiza wanafunzi wa shule hiyo na uongozi kuitunza na kuahidi kuifutilia kuona asilimia ngapi imeweza kuendelea na kukua.

Alisema tangu wameanza kampeni ya upandaji miti wameshapanda jumla ya miti 6500 na kwa upande wa Bagamoyo tayari wameshapanda katika shule tano na kuahidi kuendelea kupanda miti ili nchi iwe mahali pazuri katika eneo la mazingira.

"Tunapokuja kwa wanafunzi wanajifunza wao na ni elimu, tukihamasisha kwa kupanda wakiwa wanaona baba zao, kaka zao, dada zao na Shangazi zao wanavyofanya kutunza mazingira wanajifunza wakiwa wadogo wanamwagilia aliye darasa la kwanza akimwagilia mpaka amalize darasa la saba na kuona matokeo ya ule mti atafurahia na kuchukua elimu kwa vitendo na kupeleka nyumbani," alisema.

Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Shaibu Ndemanga aliwashukuru Standard Chartered kwa kushiriki kutoa miche hiyo na kuhimiza taasisi nyingine kuiga mazuri huku akiwataka viongozi wa halmashauri ya Bagamoyo kuweka mkakati kuhakikisha miti inayopandwa inaishi.

Alisema kampeni hiyo ili iweze kufanikiwa lazima kila mmoja ashiriki kwa maana ya wananchi, taasisi mbalimbalina kwamba wanafanya juhudi za kupanda miti kwasababu ndio njia sahihi iliyothibitika na ya uhakika ya kupambana na hewa ukaa, pia ndio maisha ya viumbe hai wanaotumia miti kuvuta hewa ya oksijeni na kabonidayoksaidi.

'Miaka 10 iliyopita kuna maeneo ya Bagamoyo yalikuwa Msitu , kuna maeneo yamevunwa sana kuliko juhudi za kupanda na kuhihifadhi hivyo, tusipopanda miti hii kutakuwa Jangwa

Tuendelee kupanda bila kuchoka na ni lazima juhudi za kupanda zizidi nguvu tuliyotumia katika kuharibu,"alisema.

Ndemanga alisema kuna watu wanachimba mchanga wanaharibu mazingira na kuagiza Halmashauri ya Bagamoyo kuhakikisha wanapotoa vibali vya watu kuchimba waingie nao mkataba kwamba wakishamaliza wafukie mashimo vinginevyo kunaweza kuchangia mabwawa yasiyokuwa na faida na ni hatari kwa watoto wanaocheza maeneo hayo.

Awali, Head of Public Sector and Financial Institution wa Standard Chartered Sapientia Balele alisema ni muhimu kulinda mazingira kwa vizazi vya sasa na vijavyo kulinda mabadiliko ya tabia nchi na kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali kusapoti miradi mbalimbali kuendelea kulinda mazingira.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo Shauri Selanda alisema katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi benki hiyo imepanda miti takribani 4500 katika shule mbalimbali za msingi kwenye Halmashauri hiyo.

Alisema Tatedo kwa kushirikiana na Halmashauri hiyo nao watapanda miti 2000 hivyo jumla itakuwa 4000 akisema shule ya Kigongoni itakuwa na mazingira mazuri ya kujisomea.

Mkuu wa Wilaya Bagamoyo, Shaibu Ndemanga, akipanda mti katika Kampeni ya upandaji miti iliyotolewa na benki ta Standard Chartered katika Shule ya Msingi Kigongoni iliyopo wilayani humo mkoani Pwani.
Mkuu wa Wilaya Bagamoyo, Shaibu Ndemanga (kushoto), Mkuu wa Uwendeshaji na mambo ya Teknorojia wa benki ya Standard Chartered, Christopher Vuhahula (kulia), wakiwakabidhi miti ya matunda nay a kivuli wanafunzi wa Shule ya Msingi Kigongoni iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani wakati wa upandaji miti iliyotolewa na benki hiyo shuleni hapo.

Mkuu wa Uwendeshaji na mambo ya Teknorojia wa benki ya Standard Chartered, Christopher Vuhahula (katikati), akipanda mti na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kigongoni iliyopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani kufuatia kampeni ya benki hiyo ya kupanda miti katika Mkoa huo ili kutunza mazingira kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Mary Musa.

Wafanyakazi wa Benki ya Standard Chartered, wakipanda miti katika eneo la Shule ya Msingi Kigongoni, iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani kufuatia Kampeni ya benki hiyo ya kupanda miti ili kutunza mazingira mkoani humo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kigongoni, iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani, wakishirikiana na wafanyakazi wa benki ya Standard Chartered, kupanda miti katika eneo la shule hiyo katika Kampeni ya benki ya kupanda miti ili kutunza mazingira mkoani humo.


 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...