Na Mwandishi wetu
TAMTHILIA ya 'Nice to Meet you' inayowakutanisha waigizaji Lulu Abas 'Lulu Diva' na Hemed Suleiman 'Hemed 'PHD' wenye uhasama kuzinduliwa rasmi Novemba 18, mwaka huu.
Wawili hao inasemekana walianza tofauti zao tangu walipokuwa lokesheni wakirekodi Tamthilia hiyo iliyowahusisha na ugomvi wao kuendelea hadi kwenye maisha yao ya kawaida.
Akizungumza na waandishi wa habari Hemed PHD alisema kuwa yeye ndio aliyebeba thamthilia hiyo ya 'Nice to meet you' itakayo kuwa inarushwa Startimes kupitia chanel ya Swahili Plus.
"Ushiriki wangu katika tamthilia hii Mimi ndio muhusika Mkuu na nimeigiza kama mtumishi wa Mungu nimeigizaje humo ndo unatakiwa kumfatilia kuanzia uzinduzi rasmi hadi tamthilia yenyewe Watanzania wajiandae kumuona Saimon Mlokole.
"Natoa shukrani zangu kwa wote tulioshirikiana ni tamthilia yenye visa na matukio mengi na mafundisho katika jamii yetu ya Tanzania,"alisema Hemed PHD.
Kwa upande wa Lulu naye pia, alisema hakutaka kukatana na Hemed na alioneshwa kuchukukizwa na kusema kitendo cha kumuona kimemkata maini na kuanza kulia lakini mwisho wa siku alizungumzia ujio wa tamthilia hiyo akisema ana imani watu wataipenda.
"Nice to meet you ni mradi mzuri, kazi nzuri watu wataipenda, tumeigiza vitu vingi,"alisema. Wasanii wote wawili wameigiza kama wahusika wakuu kwenye tamthilia hiyo.
Naye Mkurugenzi wa Masoko na Maudhui wa Startimes David Malisa alisema tamthilia hiyo itarushwa kuanzia Novemba 18, mwaka kupitia Chanel ya Swahili Plus.
Alisema ndani ya tamthilia hiyo kuna kisasi, mapenzi, maisha ya hali ya chini na kwamba ni tamthilia itakayoshika hisia za kila mtu kutokana na ujumbe uliko ndani yake.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...