Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Salim Msangi amewasilisha mada kuhusu utendaji kazi wa TCAA katika Mkutano wa 8 wa mwaka wa Jukwaa la Wahiriri Tanzania (TEF),unaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 06- 09, 2024 katika ukumbi wa NSSF Mafao House- Ilala.

Katika mada hiyo wahariri walipata fursa ya kuyafahamu kwa kina majukumu ya TCAA. Na pia walipata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali ambayo yalijibiwa na Mkurugenzi Mkuu pamoja na wataalam wa Mamlaka walioambatana naye.

Zoezi hilo la TCAA ni sehemu ya mikakati yake ya kutoa elimu kwa wadau wakuu wa vyombo vya habari inalolifanya kila mwaka.

Huu ni muendelezo wa TCAA kuutambua na kukuza ushirikiano na vyombo vya habari ambao ni wadau muhimu katika sekta ya Usafiri wa Anga nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Salim Msangi akipokea cheti cha udhamini kutoka kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania ( TEF), Deodatus Balile  wakati wa  Mkutano wa 8 wa Jukwaa la Wahiriri unaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 06- 09, 2024 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Salim Msangi akiwasilisha taarifa ya utendaji ya TCAA katika Mkutano wa 8 wa Jukwaa la Wahiriri unaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 06- 09, 2024 
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania ( TEF), Deodatus Balile akitoa neno la ukaribisho kwa viongozi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Salim Msangi  katika Mkutano wa 8 wa Jukwaa la Wahiriri unaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 06- 09, 2024 
Baadhi ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakiuliza maswali mara baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Salim Msangi kuwasilisha taarifa ya utendaji ya TCAA katika Mkutano wa 8 wa Jukwaa la Wahiriri unaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 06- 09, 2024 

Mkutano ukiendelea

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Salim Msangi akijibu baadhi ya maswali yaliyokuwa yanaulizwa na Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari mara baada ya kuwasilisha taarifa ya utendaji ya TCAA katika Mkutano wa 8 wa Jukwaa la Wahiriri unaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 06- 09, 2024 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Salim Msangi akisalimiana na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania ( TEF), Deodatus Balile  mara baada ya kuwasili kwenye  Mkutano wa 8 wa Jukwaa la Wahiriri unaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 06- 09, 2024 
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Salim Msangi wakiwa kwenye picha ya pamoja 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...