NA WILLIUM PAUL, MOSHI.

WABUNGE wa majimbo ya Moshi Vijijini Profesa Patrick Ndakidemi na wa jimbo la Vunjo Dkt. Charles Kimei na wale wa viti maalumu mkoa wa Kilimanjaro Shally Raymond na Esther Maleko wameshiriki katika hafla ya kutoa mikopo kwa vikundi 10 katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro.

Hafla hiyo, ilifanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, eneo la KDC ambapo mikopo yenye thamani ya Sh milioni 141.8 ilitolewa kwa vikundi 10 vilivyohusisha akina mama na vijana katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa serikali wa 2024/25.

Katika mikopo hiyo, shilingi Milioni 74,182,000 zilitolewa kwa vikundi 6 vya wanawake na jumla ya shilingi milioni 67,500,000 kwa vikundi vinne vya vijana.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wabunge hao waliipongeza serikali kwa kuifungua upya mikopo hiyo ambayo wamesema ni fursa itakayowawezesha wananchi kujiendeleza kiuchumi na kujikwamua kimaisha na kuwashauri wanufaika wa mikopo hiyo kuitumia kwa malengo yaliyowekwa na pia wairudishe kwa wakati ili iweze kunufaisha wananchi wengi.

Mbunge wa jimbo la Moshi vijijini, Prof. Patrick Ndakidemi alishauri wawezeshaji waweke nguvu kwenye kuwaelimisha vijana wa kiume ili waitumie vyema fursa hiyo kwani uwakilishi wao ulikuwa mdogo sana.

Akikabidhi mikopo hiyo Mkuu wa Wilaya ya Moshi James Kaji ametoa wito kwa waliokopa mikopo hiyo kuitumia kama inavyotarajiwa.

Aliwaelekeza maafisa ustawi wa jamii walioko Halmashauri ya Moshi watoe elimu kwa watu wenye ulemavu ili nao waweze kunufaika na mikopo hiyo





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...