NA FARIDA MANGUBE, MOROGORO 

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Leo Novemba 11, 2024 imetoa mafunzo ya ufuatiliaji matukio ya moto Kwa kutumia mifumo ya Satelaiti Kwa Wahifadhi wa TFS Kanda ya Mashariki yanayofanyika mjini Morogoro.

Rogers Nyinondi ni Mhifadhi Mwandamizi wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) amesema mfumo wa Satelaiti unamsaidia Mhifadhi kutambua kiashiria cha Moto akiwa sehemu yoyote Duniani hivyo ataweza kuchukua hatua za haraka kudhibiti. 

Nyinondi amesema mafunzo hayo ni sehemu ya ya mpango wa muda mrefu wa kukabiliana na matukio ya moto lengo kubwa ni kuhakikisha matukio ya moto yanathibitiwa pale yanapotokea pia kufuatilia viashiria vya moto kabla haujatokea na kuchukua tahadhari

“Ni mifumo rafiki ,kinachotakiwa ni kuwa na simu janja na kutumia mtandao na kuweza kungia na kuona matukio ya moto maeneo mbalimbali na hata kama upo jirani na hivyo kuchukua tahadhari mapema” amesema Nyinondi.

Amesema lengo la TFS ni kufikia asilia sifuri ya Misitu yote inayoungua nchini na hii baada ya kuongeza kasi ya Utoaji elimu Kwa jamii inayozunguka Misitu pamoja na kutumia teknolojia ya Setelauti.

Kwa wake Mhifadhi Mkuu Ugani na uenezi TFS Kanda ya Mashariki Shaaban Kiulah, amewataka washiriki kutumia elimu watakayoipata katika mafunzo hayo ili kudhibiti matukio ya moto katika vituo vyao vya kazi.

Kiulah  amesema TFS itaendelea kutoa elimu Kwa makundi mbalimbali lengo likiwa kudhibiti matukio ya moto katika Misitu yote hapa nchini Tanzania.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...