Tamasha la Hot Rhythm Music Festival lililofanyika katika Hostel za Mabibo siku ya jumamosi jijini Dar es Salaam, liliwaleta pamoja wanafunzi wa Chuo Kikuu kwa ajili ya kusherehekea muziki na burudani huku wakipata ladha safi ya vinywaji vya Coca-Cola.
Tamasha hilo lilivutia mamia ya wanafunzi ambao walionekana kufurahia uwepo wa chapa hiyo kubwa ya vinywaji, ambayo ilitoa msisimko wa ziada katika burudani hiyo.
Uwepo wa Kampuni ya Coca-Cola uliongeza shangwe kwani wanafunzi walipata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali na kuonja ladha murua ya kinywaji chapa ya Coca-Cola.
"Tamasha hili limekuwa la kipekee kwa sababu ya uwepo wa Coca-Cola, wametufanya tuhisi kuwa sehemu ya kitu kikubwa," alisema Riziki Asangwile, mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Vilevile, wanafunzi walishiriki michezo na mashindano mbalimbali yaliyowekwa na timu ya Coca-Cola ambayo yaliwapa washiriki nafasi ya kujipatia bidhaa na zawadi maalum. Burudani hiyo iliendelea hadi usiku huku wanafunzi wakifurahia muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali walitumbuiza usiku huo, na kufanya wikiendi ya wanafunzi walioudhuria Tamasha hilo kuwa ya kipekee.
Kwa ujumla, uwepo wa Coca-Cola katika tamasha la Hot Rhythm Music Festival ulionekana kuongeza msisimko wa ziada na kutoa burudani isiyo na kifani kwa wanafunzi wa vyuo waliokusanyika mahali hapo.
Home
BURUDANI
Wanafunzi wa Chuo Kikuu Wafurahia Uwepo wa Coca-Cola Kwenye Tamasha la Hot Rhythm Music Festival
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...