NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

WANAHARAKATI wa Jinsia na Maendeleo wameshauri kuwaunga mkono wanawake ambao wameteuliwa na vyama vyao kutokana na kukatwa majina ya  wanawake wengi katika mchakato wa ndani wa vyama vyao.

Akizungumza jana Novemba 06,2024 Mabibo-Jjijini Dar es Salaam katika ofisi za Mtandao wa jinsia TGNP kwenye semina za jinsia na Maendeleo (GDSS)zinazofanyika kila Jumatano, Mwanaharakati wa Haki za Binadamu, Nobart  Dotto amesema wao kama wanahaharakati wamedhamiria kwa dhati kuwaunga mkono wanawake walioteuliwa na vyama vyao kuanzia kipindi cha kampeni hadi katika kipindi cha kura.

Aidha Nobart ameeleza kuwa wanatamani kuona usawa wa kijinsia katika jamii ambapo wao kwa  kuonesha dhamira ya nia yao wamewaahidi wagombea hao kuwaunga mkono katika  kampeni pale zitakapo anza.

Kwa Upande wake ,Mwanaharakati wa Jinsia, Bi.Jackline Msafiri ameshauri wanawake ambao wameteuliwa na vyama vyao watambue kwamba hata kama wasipopitishwa, kura ndio zitakazo amua  hivyo wawe wavumilivu.

Aidha Jackline amewaasa wanawake waliojitoa kugombea katika uongozi, majina yao yakikatwa katika awamu hii wasikate tamaa kwani hata yeye aliwahi kugombea awali lakini alipofikia katika hatua ya uteuzi alionekana hajakidhi sifa.













Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...