Sehemu ya Magari yaliyotolewa na Amref Health Africa Tanzania kwa ajili ya kuimarisha huduma za afya katika mikoa ya Mara na Simiyu

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia afya Dkt. Grace Magembe amewaelekeza Makatibu Tawala wa Mikoa ya Mara na Simiyu kuyatunza magari wanayokabidhiwa ili yaendelee kuwahudumia wananchi katika eneo la afya kwa muda mrefu zaidi.

Dkt. Grace ameyasema hayo katika zoezi la kukabidhi magari mawili kwa Makatibu Tawala waliowakilishwa na Waganga Wakuu wa Mikoa hiyo yaliotolewa na Taasisi ya Amref Health Africa Tanzania kwaajili ya usimamizi shirikishi wa shughuli za Afya katika Mikoa hiyo katika viwanja vya TAMISEMI jijini Dodoma tarehe 11.12.2024.

“Magari haya yanapokabidhiwa kwetu tunaowajibu wa kuendelea kuyatunza na kuhakikisha yataendelea kufanya kazi vizuri ili kuhudumia wananchi” ,amesema Dkt. Grace.

Aidha Dkt. Grace ameendelea kupongeza ushirikiano uliopo kati ya Serikali na Wadau mbalimbali wakiwemo Amref Health Africa Tanzania kwa namna wamekuwa wakisaidia katika kutoa huduma mbalimbali za Afya kwa wananchi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkaazi wa Amref Health Africa Tanzania ,Dkt. Frolence Temu amesema jumla ya magari yaliyotolewa na taasisi hiyo ni sita ambapo kila mkoa unapata magari matatu.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...