Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeanza utekelezaji wa maandalizi ya matengenezo ya dharura ili kuzuia uvujaji wa maji katika maungio ya bomba la inchi 40 na inchi 28 katika Mtambo wa Uzalishaji Maji wa Ruvu Juu.

DAWASA imelazimika kuzima mtambo wa Ruvu Juu kwa saa 24 ili kuruhusu matengenezo hayo na kusababisha maeneo ya Kibaha hadi Kisarawe kukosa huduma ya maji.

Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji, Mhandisi Leonard Msenyere amesema kazi inaendelea kufanyika usiku na mchana na inategemea kukamilika ndani ya muda uliowekwa.

"Wataalam mbalimbali tunaendelea na kazi hii usiku kucha kuhakikisha inakamilika ndani ya muda uliopangwa na kuwezesha huduma kurejea kwa katika hali yake ya kawaida," amesema Mhandisi Msenyere.

Mtambo wa Ruvu Juu unahudumia maeneo ya Mlandizi, Kibaha, Ruvu Darajani, Ruvu JKT, Visiga, Maili 35, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe Saba, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Kwa Mbonde, Picha ya Ndege, Lulanzi, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Magari Saba, Mbezi Inn, Mbezi, Kimara,Tabata, Segerea, Kinyerezi, Kisukuru, Bonyokwa, Msigani, Maramba Mawili, Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti, Ubungo, Magomeni, Ukonga, Uwanja wa Ndege, Kiwalani, Vingunguti, Gongo la Mboto, Pugu na Kisarawe


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...