-Azindua Mfuko wa mikopo nafuu “SAMIA FUND”

Na Karama Kenyunko Michuzi Tv

SERIKALI imesema kuwa itazidi kuimarisha matumizi ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu hususan kwenye eneo la Utafiti ili kutatua changamoto za kiuchumi na za kijamii nchini.

Imisema wakati umefika sasa kwa Serikali na taasisi na Mashirika kutambua, kuthamini na kutumia tafiti za wanasayansi wa ndani ya nchi ili kutatua changamoto zilizopo.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amesema hayo leo Desemba 2, 2024 wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kufungua Kongamano la tisa la Sayansi, Teknolojia, Ubunifu na maonesho linaloendelea  katika ukumbi wa JNICC Jijini Dar es Salaam.

Amesema wanasayansi nchini wanafanya kazi nzuri na kubwa ya kutafuta suluhu ya matatizo mbalimbali katika jamii lakini kazi zao zinatambuliwa zaidi nje ya nchi kuliko zinavyotambuliwa nchini jambo ambalo linaweza kuwavunja moyo.

Amesema kuwa kauli mbiu ya kongmano hilo ya  matumizi ya Sayansi Teknolojia na Ubunifu katika kuhimili changamoto za mabadiliko ya tabianchi na kuchangia kwenye uchumi shinda.

"Mimi nafarijika sana kuona kauli mbiu hii inakwenda sambamba na mpango wa maendeleo wa Taifa wa ulioanzia mwaka 2021 mpaka mwaka 2026 " amesema Dkt. Biteko


Ameongeza kuwa, Kongamano hilo ni la kujadili na kutafuta suluhu ya matatizo tuliyonayo, tutumie tafiti za wanasayansi wa ndani badala ya kuwavunja moyo na kila anayejaribu kwa kutafiti apewe fursa ili aendelee kutafiti zaidi na matokeo tutayaona,” amesema DKt. Biteko.

Ameongeza kuwa Serikali inatambua mchango wa wanasayansi na kuwawezesha watafiti na wabunifu na kupitia Tume  ya Sayansi na Teknolojia COSTECH imetoa kiasi cha bilioni 32 kwa ajili ya kuimarisha miradi ya utafiti na ubunifu.

Tangu mwaka 2015 Serikali imeshapokea kiasi cha shilingi bilioni 222.8 kwa ajili ya kujenga uwezo kwa wanasayansi wabunifu kuendeleza miradi mbalimbali ambazo zimesaidia kuwajengea uwezo wanasayansi wakiwemo wanasayansi vijana.

Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia. Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali imeanza kutambua jitihada za Wanasayansi, Watafiti wa ndani ya nchi na baadhi yao wametunukiwa vyeti kwa kutambua mchango wao kwa maendeleo yaliyofikiwa katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya, Kilimo na Uvuvi.

Amefafanua kuwa njia moja yakufanya jitihada hizo kuwa endelevu, Serikali imeanzisha mfuko wa mikopo nafuu wa kubiasharisha bunifu na tafiti Tanzania unaojulikana kama Samia Fund.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Amos Nungu ameishukuru Serikali kwa uwezeshaji ambao umeiwezesha kutekeleza majukumu yake kwa viwango na kuwa moja ya taasisi mahiri ya kupigiwa mfano Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Ameongeza kuwa COSTECH kupitia program mbalimbali imewasaidia vijana wengi kubadili ndoto zao kuwa fursa ambapo pamoja na mambo mengine imefikia uwezo wa kutoa vibali 1000 kwa watafiti kutoka nje ya nchi.

Balozi wa Norway nchini, Mhe. Tine Tonnes ameipongeza Tanzania kufuatia hatua zake za kuendeleza watafiti na wabunifu huku akieleza utayari wa nchi hiyo kuendelea kuunga mkono program za uhifadhi wa mazingira.

Vikundi 19 vimepokea mfano wa hundi ya shilingi Bilioni 6.3 ikiwa ni mkopo kwa watafiti, wabunifu waliofanya kazi inayosababisha matokeo.












Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...