Katibu Mkuu Wizara ya Maji Eng. Mwajuma Waziri amemtaka Mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi wa Bwawa la Kidunda Sinohydro kuongeza kasi ya ujenzi wa mradi huo na kuukamilisha kwa wakati ili kufikia malengo ya serikali ya Awamu ya Sita ya kuhakikisha inamaliza changamoto ya huduma ya maji katika mikoa yaMorogoro, Pwani na Dar es salaam.

Eng. Mwajuma ameyasema hayo leo 06 Septemba, 2024 katika ziara yake ya kutembelea na kukagua ujenzi wa Bwawa hilo linalotarajia kuhifadhi maji kiasi cha mita za ujazo Milioni 190 pindi litakapo kamilika.

"Utekelezaji unaenda vizuri na juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan zinaonekana, fedha tayari zipo ni muda sasa wa mkandarasi kufanya kazi ili wananchi wanufaike na hili Bwawa la Kidunda" amesema 

Katika ziara hiyo Eng. Mwajuma ameambatana na Kamishina wa Bajeti kutoka Wizara ya Fedha Bw. Meshack Anyingisye ambaye amekiri kufurahishwa na kasi ya ujenzi wa mradi wa Bwawa huku akiiomba Wizara ya Maji kuendelea kuweka uangalizi wa kutosha ili mradi huu uweze kukamilika kwa wakati.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...