MENEJA EWURA Kanda ya Magharibi, Mhandisi. Walter Christopher, amewahamasisha wamiliki wa vituo vya mafuta kupeleka huduma ya nishati safi ya kupikia vijijini ili kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Mhandisi Christopher ametoa wito huo wakati wa mafunzo ya siku moja kwa wadau wa mafuta Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga .

Mhandisi Christopher amesema kuwa Serikali inaendelea kuhamasisha wananchi kutumia Nishati Safi ya kupikia ili kulinda afya, kuokoa gharama na muda sambamba na kulinda Mazingira. "Nishati Safi ya kupikia ina manufaa makubwa kwetu binadamu na mazingira kwa ujumla hivyo nawaomba wamiliki wa vituo vya mafuta muunge mkono jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kupeleka huduma hiyo kwa wananchi wa vijijini ili waweze kutumia nishati safi ya kupikia."amesema Mhandisi Christopher

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TAPSOA Wilaya ya Kahama, Bw. Alley Abeid Salum ameishukuru EWURA kwa elimu na anaamini kuwa itatoa majibu ya changamoto zinazowakabili wadau wa mafuta.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...