Meridianbet imehakikisha sikukuu inafana kwa familia zenye uhitaji katika eneo la Sinza Uzuri jijini Dar-es-salaam, Kwani leo wamefanikiwa kutoa msaada kwenye familia hizo na kurudisha tabasamu.

Sinza Uzuri jijini Dar-es-salaam ndio sehemu ambayo Meridianbet waalihakikisha wanatoa msaada wa mahitaji ya chakula kwa familia kadhaa ambazo hazina uwezo wa kutosha, Ili kuhakikisha sikukuu inaenda vizuri kwa familia hizo ambazo kimsingi ziliuhuihitaji msaada huo.

Kampuni hiyo wamefanikiwa kutoa msaada wa mchele, Sukari, mafuta ya kupikia, Unga wa sembe, bila kusahau sabauni za kufulia nyumbani ni wazi msaada huu utawasogeza mbele familia hizi kwa namna moja ama nyingine.

Huu umekua utaratibu wa Meridianbet miaka nenda rudi ambapo wamekua wakihakikisha wanagawana kile walichokipata na jamii yao, Kwani mara zote wamekua wakitaka jamii yao ifurahie uwepo wao lakini pia wakigusa zaidi wale wenye uhitaji.

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Meridianbet Bi Nancy Ingram alipata bafasi ya kuzungumza katika ugawaji wa mahitaji hayo,"Kwanza kabisa ningependa kuwashukuru kwa ukarimu wenu mlionionesha lakini pia nafurahia kuwepo hapa kujumuika na nyie kw akutoa huu msaada kwen, Nipende tu kuwaahidi jitihada zetu za kuhakikisha tunarudisha kwa jamii hazitaishia leo tutendelea kufanya hivi kila wakati”

Halikadhalika wakazi wa Sinza Uzuri nao walifurahishwa kwa namna yake kutokana na msaada ambao Meridianbet wameutoa kwao, Kwani msaada huo wa vyakula utaweza kuwavusha katika wakati huu haswa kipindi hiki cha sikukuu ambapo vitu hupanda bei.

Sasa unaweza kunyakua kitita cha shilingi milioni moja taslimu kwa kushiriki shindano la mabingwa la michezo ya kasino ya Expanse ambapo mwisho ni tarehe 31 mwezi huu wa 12 Cheza sasa leo ujinyakulie kitita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...