Na Jane Edward, Arusha 

  Kongamano la 42 la kisayansi la chama cha kitaaluma madaktari wa wanyama Tanzania, linatarajiwa kufungulia na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan  litakalohusisha Washiriki elfu mbili kutoka katika sekta za Wanyamapori na Mifugo kutoka nchi za Jumuiya ya Madola Mkoani Arusha.

Aidha Kongamano hilo  limeandaliwa na Chama cha Madaktari wa Wanyama nchini Tanzania (TVA) kwa lengo la kujadili kwa pamoja changamoto na kuona namna bora kuboresha sekta hiyo.

Profesa Esron Karimuribo ni mwenyekiti wa Chama hicho ambapo amesema   Kongamano hilo la kisayansi litakalofunguliwa na Rais Samia lina umuhimu mkubwa kwa nchi na wananchi  kudhibiti na kutokomeza magonjwa ya Wanyama .



Ameongeza kuwa kongamano hilo litaangazia maeneo muhimu ya kuishauri Serikali jinsi ya kuboresha Sekta ya Mifugo nchini ili kufanya biashara nzuri ya mifugo Kitaifa na Kimataifa ili kukuza Uchumi wa Kaya na kuongeza Pato la Taifa kwa ujumla.


Awali kabla ya kumkaribisha mwenyekiti wa chama hicho Katibu wa Chama hicho Dk. Caroline Ulomi Uronu amesema Chama hicho kilianzishwa mwaka 1982 na kila mwaka kimekuwa kikifanya Kongamano la Kisayansi na mwaka huu litakuwa Kongamano la 42 tangu kuanzishwa kwa chama hicho.

 Profesa Gabriel Shirima ni  Daktari wa mifugo na Mwanachama wa chama hicho amesema sekta ya mifugo ina mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi nchini, pia hutoa lishe bora kwa wananchi kwani vitamini ya Wanyama ndiyo ghali zaidi duniani, huongeza mapato ya familia na ajira kwa vijana.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...