Na Chalila Kibuda ,Michuzi Tv
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limesema kuwa linaendelea na ukaguzi vyombo vya usafirishaji majini kutokana na baadhi vyombo hivyo kuzidisha abiria au mizigo katika Siku kuu za mwisho wa mwaka.

Akizungumza katika ukaguzi wa Meli ya Azam Afisa Mkaguzi Mkuu wa Shirika hilo Rashid Katonga uliofanyika Bandarini jijini Dar es Salaam.

Katonga amesema kuwa katikq kipindi hiki kumekuwa na baadhi ya vyombo vya usafirishaji majini kuongeza idadi ya abiria au mizigo kutokana na kuwepo kwa uhitaji wa watu wengi kufanya safari au kusafirisha mizigo.

Amesema katika kipindi hiki TASAC imejipanga kufanya ukaguzi kwa kuangalia uwezo wa chombo na abiria wanaotakiwa na wakibaini safari inasitishwa pamoja kulipa gharama za ukiukaji wa sheria.

Aidha Amesema kuwa ukaguzi huo unakwenda pamoja na kutoa elimu kwa abiria katika kuwakumbusha wajibu wa kusafiri kwa kutumia vyombo hivyo.

Nahodha wa Azam Marine Ferouz Kassim amesema kuwa wanafuata matakwa ya sheria katika kutoa huduma za usafiri majini.

Kassim amesema kuwa TASAC kufanya ukaguzi ni jambo zuri kutokana kukumbusha wasafirishaji kuelewa wajibu katika vipindi vyote katika kulinda maisha ya wasafiri.

Aidha amesema wataendelea kutoa huduma kwa kufuata sheria zilizowekwa mamlaka pamoja kufanya ukaguzi wao binafsi wa vyombo hivyo.Afisa Mkaguzi Mkuu wa TASAC Rashid Katonga akizungumza na Manahodha wa Meli ya Azam wakati walipofika kufanya ukaguzi wa Meli hiyo inayofanya safari zake za Dar es Salaam na Zanzibar.Afisa Mkaguzi Mkuu wa TASAC Rashid Katonga akizungumza na abiria wakati ziara ya uakaguzi wa Meli ya Azam jijini Dar es SalaamNahodha wa Meli za Azam Ferouz Kassim akizungumza kuhusiana na ukaguzi wa TASAC katika Meli hiyo.Afisa Mkaguzi Mkuu wa TASAC Rashid Katonga akiangalia idadi ya abiria waliopo katika Meli na uwezo wa Meli hiyo.Afisa Mkaguzi Mkuu wa TASAC Rashid Katonga akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ukaguzi wa Meli ya Azam jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...