Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania( TET)Dkt Aneth Komba amemshukru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha upatikanaji wa vitabu vya kiada vya Elimu ya Ualimu nchini.

Ameyasema hayo leo tarehe 4/12/2024 wakati wa uzinduzi wa ugawaji wa vitabu hivyo katika Chuo cha Ualimu Vikindu kilichopo katika wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani,ambapo amesema kuwa vitabu hivi vimeandikwa kwa mara ya kwanza katika historia ya uandishi wa vitabu vya Elimu ya Ualimu nchini.

"Tunamshukuru sana Rais wetu Dkt.Samia kwa kuhakikisha walimu wanapata vitabu hivi ambavyo havikuwahi kuwepo kwenye vyuo vya ualimu nchini tunaamini vitaleta tija na kuinua ari katika ujifunzaji kwa wanachuo vyuoni" amesema Dkt.Komba.

Dkt.Komba amesema kuwa vitabu hivyo vinagawiwa kwa uwiano wa kitabu kimoja kwa mwanachuo mmoja ili kuwapa fursa ya kuvitumia kikamilifu na kwa nafasi inayofaa.

Pia Dkt.Komba amemshukuru Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda kwa usimamizi mzuri akishirikiana na makatibu wakuu wote kwa kusimiamia vyema suala zima la upatikanaji wa vitabu hivyo vya ualimu ambavyo havijawahi kuwepo nchini.

Dkt.Komba ameeleza kuwa vitabu hivyo vimeandaliwa kwa kuzingatia mtaala ulioboreshwa wa mwaka 2023 unaozingatia ujenzi wa umahiri na ujuzi unaotumia stadi za karne ya 21 katika kutatua changamoto zinazoizunguka jamii ya Watanzania.

Kwa upande wake ,Mkuu wa Chuo hicho ,Bi.Amina Tou,ameshukuru kupatiwa vitabu hivyo na kueleza kuwa vitatumika ipasavyo katika kuwapa walimu tarajali maarifa yatakayowawezesha kufanya kazi ya ualimu kwa weledi pindi watakapomaliza masomo yao.

Vitabu hivyo vya kiada vimesambazwa katika vyuo vyote vya ualimu nchi nzima.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...